Na Mwandishi wetu,TimesMajira Online
KAMATI ya Maadili ya Mawakili imeahirisha kusikiliza kesi ya kufutwa uwakili inayowakabili Mawakili, Jebra Kambole na Edson Kilatu wanaotuhumiwa kuidharau mahakama jambo ambalo ni kinyume na maadili ya mawakili.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 19, mwaka huu baada ya akidi ya Kamati hiyo kutotimia.
Kesi hiyo iyofunguliwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Oktoba 8 mwaka jana, Wakili Jebra anatuhumiwa kuidharau mahakama kwa kuchapisha maudhui katika ukurasa wake wa ‘Twitter’ kuwa ‘Kisutu Revenue Authority’ kwa tafsiri isiyo rasmi ni ‘Mamlaka ya Mapato Kisutu’.
Jebra anadaiwa kuchapisha maneno hayo baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwahukumu viongozi tisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhukumiwa kulipa faini ya sh. milioni 350 baada ya kukutwa na hatia ya makosa 12 ikiwemo kufanya maandamano yasiyokuwa na kibali.
Naye Wakili Kilatu, anatuhumiwa kwa kuchapisha maoni kwenye ukurasa wake wa ‘facebook’ Agosti 8, 2020 maoni ambayo ni ya kuikosoa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, lakini pia maoni ambayo yanaashiria kutoiheshimu mahakama, sheria na taaluma ya sheria.
Maoni hayo pia, yanadaiwa kuwa yanaashiria kuhamasisha umma usiwe na imani na mahakama.
Kutokana na mawakili hao kwa nyakati tofauti kutoa maoni yao mitandaoni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alipeleka mashtaka kwenye Kamati ya Maadili ya Mawakili, kuomba Kamati itamke kuwa mawakili hao wamekiuka maadili ya taaluma ya sheria hivyo wafutiwe uwakili.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â