Na Esther Macha,Timesmajira,Online, Mbeya
MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Afya na Ukimwi ,Stanislaus Nyongo ameipongeza Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya (MZRH) kwa matumizi ya fedha zaidi ya bilioni 12 zilizokamilisha ujenzi wa jengo la wodi ya wazazi Meta.
Amesema wameona fedha nyingi zilizoletwa zimefanya kazi kubwa miradi ni mizuri na inaridhisha japo kuwa kuna changamoto ndogo ndogo ambazo zinaweza kurekebishwa.
Akizungumzia kuhusu jengo la upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo Mwenyekiti Nyongo amesema kuwa jengo hilo ni la muda mrefu kamati itakaporudi liwe linatoa huduma kwasababu wananchi wanasubiri huduma na jengo na kusema kuwa wananchi watakuwa na tija nalo na muda mlioomba uwe hivyo na si vinginevyo .
Aidha Mwenyekiti huyo ametoa wito kwa watoa huduma kutoa elimu kwa wanaume ili waweze kupima afya zao kwani baadhi ya wanaume wanaonekana kuwa wazito kupima afya zao.
Naibu waziri wa Afya Godwin Molleli amesema kuwa ziara hiyo ya kamati inawafundisha wapi warekebishe wapi walipokosea ili ziara ijayo waweze kuboresha`zaidi ikiwemo vifaa tiba viwe vimefika kufikia Aprili na majengo kuanza kufanya kazi rasmi .
Kaimu Mganga Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya , Karume Maisara amesema kuwa suala la unyanyapaa kwenye jamii bado lipo kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi elimu bado inaendelea kutolewa kujua kuwa tatizo bado lipo na linaweza kumpata mtu yeyote katika jamii .
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato