March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kairuki,Kitila wachukua fomu za utezi wa Ubunge 

*Ni katika majimbo ya Kibamba na Ubungo

*Kairuki aishukuru Halmashauri Kuu ya CCM

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Dar

Angela Kairuki amechuku fomu ya uteuzi wa kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Kibamba huku Kitila Mkumbo akichukua  fomu   kwa ajili ya Jimbo la Ubungo,ambapo wote wawili wakipeperusha  bendera ya Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Fomu hizo zimetolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC),kupitia Msimamizi  wa Uchaguzi wa Jimbo la Kibamba na Ubungo Rosemary Mpeleta katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo,Agosti 25,2025.

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ubungo na Kibamba Rosemary Mpeleta(kushoto) akimkabidhi fomu mgombea Ubunge Jimbo la Kibamba Angela Kairuki,katika ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar-es-Salaam Agosti 25,2025

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo,Angela Kairuki, ameishukuru Halmashauri Kuu CCM Taifa kwa kumteua kupeperusha bendera ya chama hicho Jimbo la Kibamba.

Kairuki amesema yupo tayari kuwatumikia wananchi wa Kibamba bila kujali itikadi  kwa kuleta maendeleo na fursa mbalimbali ili kukuza uchumi wa Jimbo hilo.

Kwa upande wake Kitila Mkumbo,amewaomba  wananchi wa Ubungo kujitokeza kwa wingi Agosti 28,2025, Tanganyika Parks katika uzinduzi wa kampeni za CCM kitaifa.

Mbali na hao mgombea Udiwani wa CCM Kata ya Mbagala wilayani  Temeke Abdulkarimu Pazi,amesema atakaposhinda nafasi ya Udiwani atazingatia utu bila upendeleo kwani chama hicho  kinategemewa na wananchi pamoja na nchi.

Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ubungo na Kibamba Rosemary Mpeleta(kushoto) akimpa fomu mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo Kitila Mkumbo kupitia CCM, katika ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar-es-Salaam Agosti 25,2025