Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za ikoa a Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Angela Kairuki ameliasa Baraza la Wafanyakazi la Tume ya Utumishi wa Walimu kufanya kazi kwa weledi na bidii kama sehemu ya kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan hasa katika sekta ya elimu nchini.
Kairui ameyasema hayo leo Machi 16,2023 wakati wa akifungua Baraza Baraza hilo jijini Dodoma huku akisema,katika miaka miwili ya uongozi wake Ras Dtk.Samia amefanya mambo mengi na hivyo kuongeza tija katika sekta ya elimu huku kisema mafanikio hayo yaelezwe kwa kina ili watanzania wajue nini serikali yao inafanya.
“Katika kipindi hiki cha miaka miwili Rais Dkt.Samia ameendelea kutatua changamoto mbalimbali na kuhakikisha mazingira ya kufanyia kazi kwa walimu na changamoto zinazowakabili zinaendelea kutatuliwa kila siku.”alisema na kuongeza kuwa
“Shukrani kwa Rais kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya haswa katika kutoa kipaumbele kwa sekta ya Elimu na walimu wake ,tumlipe kwa kufanya kazi kwa bidii sana,tutimize wajibu wetu kwa weledi na ufanisi wa hali ya juu sana.”alisisitiza
Aidha Waziri huyo alisema,Ofisi yake inaendelea kufanyia kazi suala la kada ya Makatibu wa wilaya huku akisema muda si mrefu itapata ufumbuzi kwa makatibu hao wa wilaya wanapatikana.
Awali Katibu Mtendaji wa Tume ya Utumishi wa walimu (TSC) Paulina Mkwama alisema Rais Dkt.Samia anastahili pongezi kwa namna ambavyo amekuwa akishughulikia changamoto za watumishi wa umma hususan walimu.
“Katika kipindi kifupi cha Rais Dkt.Samia tumeshuhudia walimu wakipanda vyeo kwa mkupuo wakiwemo walimu 160,888 walipandishwa vyeo kwa mkupuo,watumishi walimu 20,032 walijiendeleza na kubadilishiwa vyeo ,
“Pia serikali imelipa malimbikizo ya madai mbalimbali ya mishara na yasiyo ya mishahara,kukabiliana na upungufu wa walimu kwa kuajiri ambapo kwa mwaka 2020/21 watumishi 14,949 na 2021/22 watumishi 9,800 .”alisema Mkwama
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini