December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kaijage agawa chakula kwa makundi maalum

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji Umoja wanawake( UWT )Wilaya ya Ilala Fanta Boniface Kaijage, amegawa chakula na Futari kwa watoto wa makundi maalum wa kituo cha watoto yatima Msongola wilayani Ilala.

MJUMBE Fanta boniface Kaijage amegawa chakula hicho na watoto yatima sehemu ya utaratibu wake endelevu ndani ya wilaya Ilala kushiriki matukio ya kijamii.

“Nimegawa vyakula mbalimbali vikiwemo mchele ,Sukari, Maharage, sembe,Mafuta ,Sabuni,juice na mikeka ya kukalia katika kituo hichi cha watoto yatima Msongola pamoja na furari lengo na dhumuni kushirikiana chakula cha pamoja nao ili na wao wajione sawa na jamii nyingine “alisema Fanta.

Fanta Boniface Kaijage alisema utaratibu huo ni endelevu katika kusaidia makundi maalum ili kuwapa faraja .

Alitoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia watoto wa makundi maalum ili na wao wajione sehemu ya jamii.

Mlezi wa Kituo cha Yatima Msongola Christina Haule, alisema kituo hicho kimeanzishwa mwaka 2004 kimesajiliwa mwaka 2006 kinapokea watoto wa aina zote kina watoto 89 .

Mlezi Chritina Haule aliwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia watoto wa makundi maalum.

Mmmoja wa watoto wa makundi Maalum wa kituo hicho Stella Poul , alisema alipokelewa katika kituo hicho akiwa Chekechea mpaka sasa anasoma shule ya Sekondari alitumia fursa hiyo kumshukuru Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji uwt wilaya ya Ilala Fanta Boniface kaijage kwa misaada aliotoa katika kituo chao.