Judith Ferdinand, Timesmajira Online
Mkurugenzi wa kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi(PPPC),David Kafulila,ametaja mambo ya msingi ya kuzingatia ili kufikia Dira ya Taifa ya 2050 ikiwa ni rasilimali watu, jiografia na diplomasi.
Hayo amebainisha wakati akizungumza katika moja ya kipindi cha kituo cha runinga,nchini hapa,ambapo Kafulila amesema, ili kufikia Dira hiyo,jambo la kwanza lazima kuwe na nguvu kazi yenye maarifa,ambayo inaweza kuzalisha, kushindana na kujenga uchumi.
Kafulila amesema,jambo jingine ni nafasi ya jiografia ya nchi kubadilisha kiuchumi kunaweza kuchangia kuliko sekta yoyote ile kwa sababu imepakaba na nyingi ambazo hazina bandari hivyo zinafanya biashara duniani kupitia Tanzania.
“Zaidi ya asilimia 80 ya biashara yote duniani inafanywa kupitia bahari,nchi ambayo ina eneo kubwa la bahari na inategemewa na nchi nyingine kufika duniani kufanya biashara ya kununua na kuuza basi nafasi hiyo ya kijiografia,hivyo sekta hii ya miundombinu inahitaji uwekezaji zaidi,”amesema Kavulila na kuongeza:
“Ndio maana Serikali imeanza kuwekeza kwenye bandari ambapo imeita sekta binafsi kuwekeza kwenye bandari ya Bagamoyo pia sekta binafsi kufanya upanuzi zaidi kwenye bandari ya Dar-es-Salaam lakini sekta itumike kwenye uendeshaji wa sehemu ya bandari hiyo.
Sababu hizi ni kufanya nchi ifaidike na nafasi ya kijiografia kujenga uchumi wake kwa sababu ni nafasi ambayo tunayo,”.
Pia amesema,jambo jingine ni diplomasia ya kiuchumi ambayo ni msingi mkubwa usioonekana sana lakini una matokeo makubwa kwani kila walipokosea kwenye eneo hilo palikuwa na athari kubwa kwenye uchumi.
“Serikali ya awamu ya sita baada ya kufungua diplomasia yake katika uchumi, biashara ya Tanzania duniani imeongezeka,mwaka 2021 mauzo na manunuzi ya nje yalikuwa takribani dola milioni 17 lakini sasa ni zaidi ya dola milioni 34, yamekwenda mara mbili,hii ni kwa sababu ya sehemu ya juhudi ya kujenga diplomasia ya kiuchumi,”.

More Stories
TAMWA yakumbusha jamii kupinga ukatili wa kijinsia kuelekea siku ta wanawake Duniani
Wanawake washauriwa kuchangamkia fursa za uchumi
Aida:Wanawake wakipata haki zote itapunguza migogoro