Ashura Jumapili,TimesMajira Online,Bukoba
Makada wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),Jimbo la Bukoba Mjini,wamajitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho, katika nafasi ya Ubunge jimboni humo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Miongoni mwa waliojitokeza kuchukua fomu ya kuwania Ubunge baada ya CCM kufungua rasmi zoezi la uchukuaji fomu Juni 28,2025, ni Mhandisi Johnston Johansen wa TANROADS Kagera ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi TANROADS kitaifa akiwasilisha Mkoa wa Kagera.
Kwa upande wa siasa ni mwanachama wa CCM, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya kutoka Kata ya Kibeta,ambapo mwaka 2015 na 2020 alichaguliwa kushiriki kampeini za Chama kwa njia ya mtandao na baada ya uchaguzi mwaka 2020 aliteuliwa kuwa mlezi CCM kyata ya Kahororo.Aidha mwaka 2020 alitia nia ya kugombea Ubunge na kwenye kura za maoni alishika nafasi ya 12 kati ya wagombea 57.

Mbali na huyo wengine waliochukua fomu katika Jimbo la Bukoba mjini ni Gofrey Benjamini maaarufu Kanyanyinyi, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Pwani, Mkurugenzi wa kiwanda cha kukoboa kahawa Amri Amza pamoja na Almasoud Kamala aliyeshika nafasi ya kwanza katika kura za maoni Mwaka 2020.
Pia Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa mkutano mkuu wa CCM Wilaya ya Karagwe kutoka Tawi la Rwambaizi, Mwalimu Prince Bashaija Rwazo, amechuku fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Karagwe.Ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika linalowasaidia wanawake na watoto katika Maswala ya kisheria ya Rwazo Foundation .

Hata hivyo Katibu wa Itikadi,Hamasa,Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Kagera Hamim Mhamudu, amesema kuwa ofisi zote za CCM zitakuwa wazi kuanzia saa 2 hadi saa 10,jioni na zoezi litahitimishaa Julai 2,2025,ambapo ametoa wito kwa kila mwenye sifa za chama kwa ngazi ya Udiwani na Ubunge kufika katika maeneo husika kuchukua fomu.


More Stories
Wanawake washauriwa kuchangamkia fursa za uchumi
Aida:Wanawake wakipata haki zote itapunguza migogoro
LGTI wanawake waadhimisha siku yao Ngorongoro