January 20, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kada wa CCM ajingonga

Na Moses Ng’wat, TimesMajira Online, Mbozi.

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mlowo, Wilayani Mbozi, Misheck Mwambogolo, (47) amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya manila shambani kwake .

Mwambogolo ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Msingi cha ushrika (Amcos) cha Shimondo, Wilayani hapa, anadaiwa kujinyonga kutokana na masuala ya biashara ya Kahawa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya, akizungumzia tukio hilo leo Jumatatu, Aprili 24, 203 amesema lilitokea saa 7:00 usiku baada ya kukutwa akiwa amejinyony
onga juu ya mti kwa kutumia kamba ya manila.

Kamanda Mallya amesema marehemu aliacha ujumbe wa maandishi kwenye gari yake, kama unavyosomeka kwenye taarifa ya jeshi hilo la polisi Mkoa wa Songwe.