December 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kada Kaniki atatua kero Zingiziwa

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

KADA wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala Selemani Kaniki anetatua kero sugu kwa wananchi wa Mtaa wa Zogoali kwa kujitolea KALAVATI mbili kwa wananchi wa mtaa wa Zogoali Zingiziwa wilayani Ilala.

Kada Selemani Kaniki alitoa KALAVATI hizo mbili leo Mei 11/2024 ambapo awali alisaidia Serikali kwa kutoa kalavati nne mpaka sasa zimefikia KALAVATI sita ikiwa sehemu ya mchango wake .

Akizungumza mara baada makabidhiano hayo Selemani Kaniki alisema kero hiyo ni zaidi ya miaka kumi ndio imetatuliwa leo kivuko kwa Mama Yusuph ambapo vifaa vyake vicenza kumalizika hivi karibuni ujenzi wake utaanza rasmi.

“Nimekabidhi KALAVATI nne awali na leo nimekabidhi KALAVATI mbili jumla KALAVATI sita kwa ajili ya kuisaidia Serikali na Chama cha Mapinduzi CCM katika kutatua kero za wananchi ndani ya wilaya yote ya Ilala ujenzi wake utaanza hivi karibuni “alisema Kaniki.

Kada Selemani Kaniki alisema yeye zaidi yupo katika utekelezaji wa Ilani ya chama na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan mwaka 2025 tunaenda na mama mitano tena katika ngazi ya Urais.