Na Penina Malundo.
JUMUIYA ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) imesema itaendelea kumuenzi na kumkumbuka aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara kariakoo Shaabani Makongoro aliyefariki Dunia April 16 mwaka huu.
Mwenyekiti huyo alifariki katika hospitali ya Rabininsia Tegeta jijini Dar es Salaam na kuacha pigo kubwa kwa wafanyabiashara wa kariakoo.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya habari na mawasiliano kupitia Ofisa habari wa JWT , Stephen Chamle alisema Marehemu alifariki katika hospitali hiyo na taratibu za mazishi zinatarajia kufanyika leo kwa kuupumzisha mwili wa marehemu katika makaburi ya kondo Tegeta.
Alisema Marehemu alikuwa mfanyabiashara wa Kariakoo, Mtaa wa Mchikichi na Sikukuuu jijini Dar es Salaam, ambapo alikuwa mwenyekiti wa wauzaji wa urembo kwa miaka minne na baadae March 2019 aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara kariakoo.
“Marehemu Shabaani Makongoro mpaka anafikiwa na umauti alikuwa Mtu mwenye moyo wa kuunganisha watu lakini pia alihakisha wafanyabiashara wa kariakoo wanakuwa na ushirikiano mzuri na serikali hatua iliyopelekea uchumi na maendeleo ya Mkoa wa Dar es salaama Taifa kwa ujumla kuimarika,” ilisema taarifa hiyo
Aidha ilisema kabla ya Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kariakoo aliwahi kushika nafasi ya Mwenyekiti wa wauzaji wa urembo Kariakoo kwa takribani miaka minne na kuja kuwa mjumbe wa JWT kisha kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa wafanyabiashara kariakoo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
More Stories
Prof.Muhongo awapongeza vijana 32 waliotembea kwa miguu kutoka Butiama hadi Mwanza
Rais Samia atimiza ahadi Hanang
Daktari Dar ajishindia Mil. 100/- za Fainali NMB Bonge la Mpango