TORONTO, Canada
MSANII wa muziki wa Pop na R&B kutoka nchini Canada, Justin Bieber ametajwa kuwania Tuzo za Grammy 2021, katika Vipengele vinne ambavyo ni ‘Best Pop Vocal Album’, ‘Best Pop Solo Performance’, ‘Best Pop/Duo Group Performance’ na ‘Best Country Duo/Group Performance’,
Hata hivyo, licha ya kutajwa kwenye orodha hiyo lakini msanii huyo, amewakosoa waandaaji wa tuzo hizo kuwa wameweka kipingele cha Best pop vocal album’ wakati albam hiyo ni ya R&B.
Akiweka wazi hilo, Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram Bieber alishangazwa na kitendo cha waandaaji wa hao kuiweka album yake ya ‘CHANGES’ katika vipengele tofauti.
Bieber amewataka watu wasitafsiri vibaya alichokisema kwani hayo ni mawazo yake mbayo mtu anaweza kukubaliana nayo au kuyakataa na pia, amewashukuru watu wote waliomuwezesha kutajwa kuwania Tuzo katika vipengele hivyo.
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio