Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
JUMUIYA ya Wazazi Wilaya ya Ilala yaunda Kamati ya ushindi ya watu 15 kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024 ili kuakikisha chama cha Mapinduzi CCM kinashika dola
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Ilala Mohamed Msophe, wakati wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Ilala.
“JUMUIYA ya Wazazi wilaya ya Ilala inatarajia kuunda timu za ushindi za watu 15 kuakikisha ccm inashika dola katika chaguzi zake zote za Serikali ya mtaa katika mitaa 159 Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam “alisema Msophe.
Mwenyekiti wa Wazazi Mohamed Msophe, aliwataka makatibu wa Jumuiya ya Wazazi wa Matawi kujenga mahusiano mazuri katika jamii ikiwemo makundi maalum pamoja na vijana wa Bodaboda .
Aidha alisema Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Ilala mikakati yake sasa hivi kuanza ziara ya matawi kwenda kuelezea yake mazuri ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM yaliofanywa na Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ,ikiwemo miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya na sekta ya Elimu.
Katika hatua nyingine alisema kila mtu anayo haki ya kugombea hivyo wasubiri mda ufike wasianze kampeni mapema wasubiri filimbi ya uchaguzi itakapoanza ndio waanze kampeni za uchaguzi kupitia ccm.
Aidha aliwataka makatibu wa chama cha Mapinduzi kujenga mahusiano mazuri na viongozi wa Jumuiya ya Wazazi ccm ili kuakikisha Jumuiya hiyo inafikia malengo yake .
Wakati huo huo Jumuiya ya Wazazi walitoa vyeti vya shukrani wadau waliochangia mkutano mkuu wa Wazazi pamoja na zawadi Maalum kwa Mbunge wa jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli, Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu ,Mbunge wa Ukonga Jery Silaa ,Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo na Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Albert John Chalamila
More Stories
Prof.Muhongo awapongeza vijana 32 waliotembea kwa miguu kutoka Butiama hadi Mwanza
Rais Samia atimiza ahadi Hanang
Daktari Dar ajishindia Mil. 100/- za Fainali NMB Bonge la Mpango