January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jumuiya ya Wazazi watoa tamko kuelekea uchaguzi 2024

Na Herishaban, TimesMajira Online, Ilala

Jumuiya ya Wazazi ya chama cha Mapunduzi(CCM) Taifa imewataka jumuiya ya Wazazi wasianze chokochoko mapema kufanya kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa kabla wakati wake.

Hayo yalisemwa na Mjumbe wa Baraza la Jumuiya ya Wazazi viti vitatu Bara Ally Mandai, wakati wa mafunzo kwa viongozi wa jumuiya ya Wazazi ngazi kata na matawi iliyowashirikisha kamati tendaji za matawi mafunzo yalioandaliwa na Kamati ya Utekelezaji ya wilaya Ilala.

“Naomba kila kiongozi wa jumuiya atekeleze ilani katika maeneo yake na kusimamia miongozo muda ukifika mchague kiongozi sahihi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024 msiache hata mtaa mmoja alisema Mandai.

Mjumbe wa Baraza la Wazazi Taifa Mandai aliwataka Jumuiya ya wazazi waandae Kiongozi sahihi anayekubalika kwa wananchi ndani na nje ya chama wasipoteze muda wa kuvutana mashati aliwataka washirikiane katika chama katika utekelezaji wa Ilani na kusimamia miradi ya maendeleo ya Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Alisema dhumuni la kupewa mafunzo na Kamati ya utekelezaji ya jumuiya ya Wazazi wilaya ya Ilala viongozi wa Matawi ,kata mpaka Taifa ambapo alisema baada mafunzo hayo kazi yao itakuwa nzuri katika utekelezaji wa majukumu yao.

Aliwataka sasa wasibweteke badala yake wafanye vikao vya msingi wa chama na kufuata miongozo waliopewa.

Katibu wa siasa na Uenezi ya chama cha Mapunduzi CCM mkoa Dar es Salaam, Ally Mananga, amewataka wanachama wa Jumuiya ya Wazazi ya ccm kuchagua viongozi wachapa kazi kwa ajili ya kushika dola wasichague kiongozi wa pesa ambaye atakuwa mzigo .

Mwenezi wa Mkoa Ally Mananga aliitaka jumuiya ya wazazi kumuunga mkono mgombea atakayepitishwa na vikao kwa ajili ya kushika dola .

Aidha aliwataka viongozi wa Jumuiya ya wazazi ngazi ya Kata na matawi wawe na nidhamu na kusimamia chama cha Mapunduzi kiweze kushika dola .

Mjumbe wa Baraza la Wazazi ccm Taifa Viti vitatu bara Ally Mandai akikabidhi mpango wa mafunzo kwa viongozi wa Jumuiya ya Wazazi kata wilaya ya Ilala mkutano ulioandaliwa na kamati ya utekelezaji wilaya Ilala (Picha na Heri shaaban)