January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jumuiya ya Wazazi Lubakaya kuongeza wanachama 800

Na Heri Shaaban , TimesMajira Online

Jumuiya ya Wazazi Lubakaya Kata ya Zingiziwa wamejipanga na mikakati yao kuongeza wanachama wapya 800 katika tawi hilo.

Hayo yalisemwa na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Lubakaya Rehema Dastun Mlenga wakati wa mkutano mkuu wa jumuiya ya Wazazi tawi.

“Jumuiya ya Wazazi tawi la Lubakaya tumepata mafanikio makubwa tumetunukiwa cheti na Junuiya ya wazazi Wilaya ya Ilala kwa kuongoza Kitaifa kwa kuingiza wanachama katika mfumo wa kadi za kisasa za electonic kutokana na ufanyaji wa kazi nzuri “alisema Mlenga.

Katibu Rehema Mlenga alisema kwa sasa mikakati yao wamejipanga kuongeza wanachama wapya 800 mpaka kufikia octoba mwaka huu kwa ajili ya kujenga chama na kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani mwaka 2025.

Akizungumzia changamoto alisema jumuiya ya Wazazi Lubakaya aina mradi wa Jumuiya wakiwa na shughuli pesa wanatoa mfukoni kwao wakikwama shughuli za jumuiya zinakwama changamoto nyingine kadi za kisasa za electonic zinachelewa kutoka kwa wakati.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tawi la Lubakaya Augustine Mwita Mseti alisema Jumuiya ya Wazazi tawi la Lubakaya linaendelea kufanya kazi zake kwa mujibu wa kanuni na katiba ya chama ili kufikia malengo yake .

Aidha Mwenyekiti Mwita alitumia fursa hiyo kuwashukuru wajumbe wa mashina kwa ushirikiano wao mzuri wanaotoa katika jumuiya ya Wazazi pamoja na chama tawi la Lubakaya pamoja na Diwani wa Kata ya Zingiziwa Maige Maganga.