January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jumuiya ya wazazi Ilala yatoa Onyo kuelekea uchaguzi wa Chama na Jumuiya

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

JUMUIYA ya Wazazi Wilaya ya Ilala imetoa onyo kwa makatibu na Wenyeviti ngazi ya Kata na Matawi wasimamie Uchaguzi vizuri bila kukata majina.

Agizo hilo limetolewa katika ziara ya Kamati ya Utekelezaji Wilaya llala na Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya llala, MOHAMED MSOPHE, wakati wa mkutano wa wanachama ukumbi wa mikutano check pont Ukonga wakati wa kutoa elimu ya Sensa ya makazi, Kuhamashisha wanachama kujisajili katika mfumo wa kielectronik pamoja na elimu ya korona na Uchaguzi ndani ya chama.

Mwenyekiti MSOPHE alisema kila mtu anayo haki ya kugombea ndani ya Jumuiya ya wazazi hivyo makatibu wa Kata na Matawi isiwe chanzo Cha malalamiko ya kukata majina yakapelekea kuvuruga Uchaguzi wa wazazi.

“Nawaomba WENYEVITI kutenda haki kusimamia uchaguzi wa tawi vizuri mrudishe majina msikate majina bila sababu za Msingi” alisema Msophe.

Msophe alisema uongozi unapangwa na Mungu kila mtu anayo haki ya kugombea uongozi anaoitaji Wananchi ndio watamuukumu.

Aidha Mwenyekiti Msophe aliwamasisha wanachama wa Jumuiya ya Wazazi kujisajili katika mfumo wa kielectronik kadi za Jumuiya ya Wazazi Ili waweze kushiriki kupiga kura.

Aliwataka wajenge Jumuiya ya Wazazi vizuri na kuweka mikakati mbalimbali ikiwemo kubuni miradi ya Jumuiya .

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Wazazi Wilaya SHAMSUDN HEMED alizungumzia elimu ya Sensa ya makazi akiwataka makatibu wa Jumuiya hiyo na Wanachama kutoa elimu hiyo na kuwa BALOZI wa mwezake Wananchi washiriki sensa kwa Maendeleo ya Taifa.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Wilaya Miraji Kibuba ametoa agizo kwa MAKATIBU Tawi MAKATIBU kata na Kamati za Utekelezaji wasim ame wenyewe kutoa fomu katika uchaguzi wao.

Kibuba alitoa onyo wasipange safi katika Uchaguzi wa wazazi wakapatikana viongozi si sahihi ndani ya Jumuiya hiyo.

Mwenyekiti wa jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Mohamed Msophe akizungumza na makatibu tawi pamoja na Kata Msongola Wilaya ya Ilala Leo Machi 29/2022 katika ziara ya kuwamasisha wanachama wa CCM wajisajili katika mfumo wa kielectronik pamoja na Elimu ya Sensa na korona (PICHA NA HERI SHAABAN)
Katibu wa Wazazi Kata ya Msongola (kulia) akikabidhiwa fomu za Uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi na Kaimu Katibu Wazazi Jamila Simba Leo MACHI 29/2022 Msongola Kitonga (Picha Na HERI SHAABAN)
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Abdalah Othiman akizungumza na viongozi wa matawi na Kata jumuiya hiyo Leo. Machi 29/2022 Msongola katika ziara ya Kamati ya Utekelezaji (PICHA NA HERI SHAABAN)
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Ilala SHAMSUDN HEMED akitoa Elimu ya umuhinu wa Sensa ya Makazi katika kikao cha Jumuiya hiyo Kata Msongola Leo Machi 29/2022 ZIARA hiyo imeandaliwa na Kamati ya Utekelezaji (kushoto) Mjumbe wa Kamati hiyo Abdalah Othiman na Kutoka (Kulia) Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya Mohamed Msophe na Kaimu Katibu Wazazi Jamila Simba (PICHA NA HERI SHAABAN)