Na Heri Shaaban
JUMUIYA ya Wazazi Wilaya ya Ilala inatarajia kuandaa mafunzo ya Wajasiriamali wote ili wajukwamue kiuchumi kwa kuwapa elimu na mafunzo mbalimbali .
Mafunzo hayo yanatolewa bure kwa wanachama wote wa Jumuiya hiyo kwa ajili ya kuwawezesha kujikwamua kiuchumi wawe na mitaji yao waendeshe familia ikiwemo kusomesha .
“Jumuiya yetu ya Wazazi Wilaya ya Ilala mikakati yake kuwapa elimu wanachama wake ya Ujasiriamari ili wajikwamue kiuchumi waweze kupata kipato kuendesha maisha na kusomesha watoto” alisema Msophe.
Mwenyekiti Msophe alisema dhumuni la mafunzo hayo kujenga chama pamoja na Jumuiya ya Wazazi kushirikiana kwa pamoja katika kutetea na kulinda dola nyakati za uchaguzi wa dola.
Alitaja mafunzo hayo yatakayotolewa na Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala alisema kuwa ni Kutengeza Mkaa kwa kutumia taka,kutengeza Sabuni,ufugaji kuku,sabuni,Batiki upambaji utengezaji keki,kupika mikate,Kilimo cha mboga mboga,elimu kwa vikundi .
Mwenyekiti Msophe aliwataka wanachama wa Jumuiya ya Wazazi kila kata kujisajili katika matawi yao watambulike kwa ajili ya mafunzo hayo yatakayotolewa bure kwa wanachama wote wa Wilaya nzima
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2021/11/WhatsApp-Image-2021-11-28-at-2.57.33-PM-1024x680.jpeg)
More Stories
Dkt.bingwa wa watoto aikabidhi Hospitali ya Kanda Mbeya mashine mbili za kutoa dawa
Askari watatu wa TANAPA wafukuzwa kazi kwa tuhuma za rushwa
Wasira: CCM itashinda dola kwa kura si kwa bunduki