Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Baada ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake Mohammed Ali Kawaida kuitaka Serikali kupitia Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kufungia Mtandao wa X ambao Zamani ulijulikana kama Twitter kutokana na mtandao huo kuruhusu mambo ambayo ni kinyume na Utamaduni wa Watanzania
Leo Juni 12,2024, Jukwaa la wanahabari wa mitandao ya Kijamii Tanzania(JUMIKITA) likiongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Ndg.Shabani Matwebe limeiomba Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Uongozi makini wa Dkt.Samia Suluhu Hassan kutokubali kamwe kuingia kwenye mtego wa kufungia mtandao huo wa Kijamii
“Ni kama ilivyo Instagram ,Facebook na YouTube, ‘x’ au Twitter ni sehemu ambayo vijana wa Kitanzania wamekua wakilitumia Jukwaa hilo kujipatia riziki mfano Matangazo lakini pia hata Kazi nzuri za Serikali mbalimbali Wanahabari wa mtandaoni wamekua wakizichapisha ‘x’ “
Taarifa ya Jukwaa imeongeza kua
“JUMIKITA ipo tayari kushirikiana na Serikali kujua namna bora ya matumizi ya mitandao ya kijamii na inatoa ushauri serikali isiingie kwenye mtego wa kufungia mtandao huo”
Jukwaa la Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA)
More Stories
Watoto wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Wananchi Kisondela waishukuru serikali ujenzi shule ya ufundi ya Amali
RC.Makongoro ataka miradi itekelezwe kwa viwango