January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Juhudi za Rais Samia zang’arisha sekta ya maji

Na Mwandishi WetuTimesmajiraOnline

WAZIRI Wa Maji Jumaa Aweso, amezindua Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Maji na kuwataka wahakikishe wanafanya kazi kwa upendo na ushirikiano ili kuleta mafanikio.

Amesema Sekta ya Maji imepiga hatua kubwa kutokana na ushirikiano ambao umejengwa na kukuzwa na Rais Samia Saluhu Hassan, ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji.

Amesema viongozi wa Sekta ya Maji wanatambua jitihada kubwa zinazofanywa na watumishi wa wizara katika kuhakikisha huduma ya majisafi na salama inafikishwa kwa Watanzania na kwamba wataendela kuongoza kwa kuhakikisha mazingira ya kazi yanaendelea kuboreshwa kwa watumishi ili kupata matokeo.

Amesema yapo mafanikio mengi ambayo wizara inapaswa kujivunia na kwamba hayo yote yametokana na ushirikiano mkubwa ambao wanapaswa kuuendeleza baina yao katika ngazi zote.

Baraza la Wafanyakazi limehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri, (ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza) na Naibu Katibu Mkuu, Agnes Meena ambao wote kwa pamoja wamewahakikishia wafanyakazi wataendela kuhakikisha kila mtumishi anapata haki yake na kuwekewa mazingira mazuri ya kutekeleza majukumu ya kazi kwa ubora unaotakiwa.