January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

JKT yajivunia mafanikio uzalishaji miaka 60 baada ya uhuru

Na Joyce Kasiki,Kilombero

MKUU wa Tawi la Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Hassan Mabena ,katika kuelekea miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara ,Jeshi hilo linajivunia katika malezi ya vijana Malezi ya vijana na maendeleo katika uzalishaji hususan wa mazao mbalimbali.

Akizingumza na waandishi wa habari katika kikosi 837 KJ,Chita JKT kilichopo katika kijiji cha Chita,wilaya Kilombero mkoani Morogoro,Brigedia Jenerali Mabena amesema,katika kipindi hicho JKT limechangia katika kuwabadiluisha vijana na kuwafanya kuwa wazalendo kwa Taifa lao.

“Sote tunafahamu kuwa tarehe 9 Disemba  nchi yetu itafikisha miaka 60 toka kujinasua kwa wakoloni,katika kuhakikisha kwamba tumechangia katika maendeleo na kuwadilisha vijana kifikra  na kuwafanya walipende Taifa lao,vijana wamefundishwa uzalendo na kipenda nchi yao.”amesema Brigedia Jenerali Mabena

Mbali na hilo amesema,JKT limekuwa likifamya shughuli zake pia kwa kutekeleza maagizo ya Serikali ambapo katika hilo limekuwa likitekeleza miradi mbalimbali ya kilimo ,mifugo na uvuvi ili kuongeza uzalishaji katika maeneo hayo.

Amesema,katika miaka 60 baada ya Uhuru,JKT limefanikiwa kuongeza uzalishaji  maradufu na kwamba hadi kufikia Mwaka 2024/2025  JKT litakuwa limeweza kujitosheleza kwa chakula.

Vile vile amesema,chakula kitakachobakia kitapelekwa  ghala kuu la serikali na kuwafikia watanzania wote hivyo kuwa na uhakika wa chakula  kilicholimwa ndani ya nchi yao.

“Na katika kipindi hicho JKT litakuwa limelima zaidi ya ekari 26,000 katika mashamba yote ya JKT.”amesisitiza

Akitoa takwimu za uzalishaji kiongozi huyo amesema,kipindi cha nyuma Jeshi hilo lilikuwa likivuna gunia tatu hadi tano kwa ekari tofauti na sasa ambapo na sasa ambapo mavuno ni  gunia kumi kwa ekari.

“Na kwa kadri tunavyoendelea na kufuata taratibu za kilimo kwa kuwahusisha wataalam wetu,malengo  ni kutoka hapo na kuzalisha hadi gunia 30 kwa ekari.”amesema

Brigedia Jenerali Mabena alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya JKT katika miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambapo akiwa katika skimu ya umwagiliaji ya zao la mpunga linalolimwa katika kikosi cha 837 KJ,Chita JKT amesema , malengo ni kulima ekari 12,000 za mpunga ambazo zitakuwa zikilimwa mara mbili kwa mwaka yaani masika na kiangazi.