December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

JKT yaita wananchi kujifunza kilimo,ufugaji wenye tija

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online , Mbeya

JESHI la kujenga Taifa (JKT) limewataka wananchi kujitokeza katika maonyesho ya kitaifa ya Nane Nane yanayoendelea jijini Mbeya ili wapate elimu katika shamba Darasa la Jeshi hilo la mazao mbalimbali kwa lengo la kuwa na kilimo chenye tija.

Akizungumza mara baada ya kutembelea shamba hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la uzalishaji Mali (SUMA JKT) Kanali Petro Ngata amesema jamii inapaswa kwenda kujifunza katika banda hilo ili kujifunza kilimo biashara na kuachana na kilimo cha mazoea.

Amesema kuwa Jeshi hilo liko mstari wa mbele kuhakikisha wanafanya kilimo bora chenye mfano kwa jamii mdio maana.wameweka shamba darasa ili wananchi waje wajifunze kilimo bora na chenye tija.

“Naomba wanamchi jitokezeni katika darasa la JKT lenye mazao mchanganyiko ambalo wanaweza kujifunza ili wakalime katika maeneo yao,”alisema Kanali Ngata.

Akizungumzia kuhusiana na ongezeko la bajeti kwenye sekta ya kilimo alisema itasaidia kupanua wigo kwenye sekta hiyo ili wakulima wazidi kupiga hatua na kufanya kilimo chenye tija.

Kwa mujibu wa Kanali Ngata, wakulima wanapaswa kuwa mstari wa mbele kupata elimu ya namna ya upandaji mazao ya mboga na mengine.ili wafanye kilimo chenye tija.

Amesema.wakifanya hivyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa uzalishaji mkubwa katika mazao mbalimbali yakiwemo ya mazao ya chakula kama mahindi,Mpunga na mengine.

Naye Mkurugenzi wa Kilimo Mifugo na Uvuvi wa JKT Kanali Peter Lushika amesema JKT ipo mstari wa mbele na kuhakikisha  kilimo wanachofanya kinakuwa na maslahi kwa jeshi hilo na Taifa kwa ujumla.

“Haturudi nyuma kwenye kilimo kila iitwapo leo,tunazidi kusonga mbele kutokana na teknolojia tunayotumia kwenye kilimo,”amesema Kanali Lushika.

Amesema wameahiriki katika maonyesho hayo ili kuweza kutoa elimu lwa wakula na wafugaji kutokana na wao kuwa webobea katika sekta hiyo.

Kanali Rushika alisema wamekuja na teknolojia mpya ya namna ya ufugaji wa samaki katika mabwawa,Vizimba na mabwawa na matenki na la kufanya hivyo ni pamoja na.kiwaaogezea hudua ya upatikanaji wa samaki aina ya sato kwa urahisi katika maeneo mbalimbali tofauti na kusubiri sato kutoka mkoa wa Mwanza pekee.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya maonyesho ya Nane Nane JKT Kanali Shija Lupi ametoa wito kwa wakulima kufika katika shamba darasa la JKT ili kujifunza namna ya utunzaji wa mazao tokea kupanda hadi kuvuna.

Teknolojia wanayofundisha wakula wanaotembelea katika banda hilo,itawasaidia kwa kiasi kikubwa kupiga hatua katika kilimo wanachofanya.