September 18, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

‎JKT yafunga rasmi mafunzo ya vijana kundi

‎Na Mwandishi Wetu

‎MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele, leo Septemba 18, 2026, amehitimisha rasmi mafunzo ya JKT kwa vijana wa Kundi la Mujibu wa Sheria, Operesheni Linda Amani, na Kundi la Kujitolea, Operesheni Nishati Safi.

‎Mafunzo hayo yamefungwa katika Kikosi cha Kanembwa JKT, Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, ikiwa ni hatua inayohitimisha rasmi mchakato wa mafunzo kwa vijana hao katika kambi mbalimbali nchini.

‎Ufungaji wa mafunzo katika kambi mbalimbali za JKT ulianza Septemba 8, 2026, ambapo sherehe zilifanyika kwa tarehe tofauti kulingana na ratiba ya kila kambi.

‎Katika baadhi ya kambi, Meja Jenerali Mabele aliwakilishwa na viongozi wengine wa JKT katika hafla za ufungaji, huku leo akiongoza mwenyewe hafla ya mwisho katika Kikosi cha Kanembwa.

‎JKT leo wanahitimisha rasmi mafunzo ya vijana wote waliokuwa katika kambi zote nchini na hafla ya Kakonko ni tukio la ujumla kwa niaba ya vikosi vyote vilivyokuwa vikiendesha mafunzo nchini.
‎xxxx