December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

JKT yaadhimisha miaka 60 kwa kuchangia damu

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

JESHI la Kujega Taifa (JKT) linaendesha zoezi la kuchangia damu kwa siku mbili ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT tangu kuanzishwa kwake .

Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya SUMAJKT House jijini Dodoma ,Mkuu wa Huduma za Sheria Makao Makuu JKT Kanali Projest Rutahiwa amesema,zoezi hilo limeanza Julai 7 na litakamilika Julai 8 mwaka huu huku akiwaasa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hilo linalolenga kuokoa maisha ya wanaohitjai kuogezewa damu.

“Tupo katika wiki ya maadhimisho ya miaka 60 ya JKT,hivyo leo na kesho Maafisa ,Askari na vijana wetu kutoka JKT 834 Makutupora tunajitolea damu kwa ajili ya wahitaj,vijana hawa wanafundishwa uzalendo na wameanza kuonyesha kwamba wao ni wazalendo,

“JKT ni mdau na mshiriki muhimu katika jamii na hapa linaonyesha mfano kwamba lipo bega kwa began a serikali katika kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wahitaji .”amesema Kanali Rutahiwa

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba JKT Meja Dkt.Yusuf Sasamalo amesema,zoezi hilo pia linaendelea katika makambi yote ya JKT huku akisema wamekadiria kukusanya chupa zaidi ya 10,000 za damu huku katika viwanja vya SUMAJKT House wakikadiria kukusanya chupa 500.

Naye Mkuu wa Kituo cha Damu salama hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) Kucy Michael amesema,umuhimu wa damu ni mkubwa katika kuchangia maisha ya watu wanaohitaji kuongezewa damu hasa watoto wadogo walio na umri chini ya miaka mitano.

“JKT wametambua umuhimu wa damu ,wapo watoto wenye umri chini ya miaka mitano wameshambuliwa na Selimundu wanahitaji damu,

“Damu ni muhimu maana hakuna kisima cha kuchota damu ,natoa rai kwa jamii iendelee kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha hasa watoto ambao wana uhitaji mkubwa wa damu.”amesema Michael