November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

JKT, Wizara ya Kilimo wasaini mkataba wa mashirikiano kuinua sekta ya kilimo

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) na Wizara ya Kilimo wametiliana saini mkataba wa mashirikiano katika kutekeleza miradi ya kilimo inayofanywa na Jeshi hilo kwa lengo la kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao hayo.

Katibu Mkuu wa Kilimo Gerald Kusaya (kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge wakisaini Mkataba wa makubaliano katika kuendeleza shughuli za kilimo zinazofanywa na JKT.Mpigapicha Wetu

Makubaliano hayo yametiwa saini na Mkuu wa JKT Meja Jenerali Charles Mbuge na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya.

Akizungumza katika ofisi za Mako Makuu ya JKT Chamwino jijini Dodoma kabla ya kutiliana saini katika mkataba huo Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Mbuge amesema,Wizara hiyo haitajuta kuingia nao katika Mashirikiano hayo.

Amesema,makubaliano hayo ni kwa ajili ya mustakabali wa nchi kupitia sekta ya kilimo ambacho ndio uti wa mgongo .

Aidha amesema mashirikiano hayo yatatoa fursa kwa vijana wengi wanaopitia JKT kujifunza na kuwa mabalozi wa kupeleka elimu ya kilimo bora kwa jamii mara baada ya kumaliza mkataba wao.

“Hapa nchini kilimo kinahusisha matabaka ya wenye nacho na wasio nacho ,na sisi JKT tunapokea vijana kutoka pande zote za nchi na baada ya kumaliza mkataba wao wanarudi katika mikoa waliyotoka kwa hiyo,kwa fursa hiyo wqtakuwa mabalozi wazuri katika maeneo yao kuelimisha wengine na hatimaye kuongeza tija katika kilimo.” Amesema Meja Jenerali Mbunge

Aidha Mkuu huyo wa JKT amemuomba Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Gerald Kusaya kutembelea skimu ya umwagiliaji iliyopo katika kikosi 837 KJ Chita ili akajionee kazi inayofanywa na JKT katika eneo hilo amvalo wamelenga kuzalisha mpunga mara mbili kwa mwaka.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Kusaya amesema mashirikiano hayo yanakwenda kutimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kutaka kufanya kazi kwa Karibu na JKT kutoka na na shughuli wanazozifanya ili kuongeza tija zaidi.

“Maono niliyo nayo sasa ndio wakati mzuri wa kulifanya JKT ling’are zaidi “amesema Kusaya.

Amesema katika mashirikiano hayo kutakuwa na muongozo ili kuwa Na mabadiliko endelevu katika sekta ya kilimo ambapo amesema makubaliano hayo ni ya miaka mitano mitano .

Pia amesema lengo la mabadiliko hayo ni kuinua pato la Taifa na hatimaye kumuinua kila Mtanzania .

“Pia katika makubaliano haya maeneo ambayo tumekubaliana ni katika kuwa na Teknolojia bora ya uzalishaji wa mazao,kujenga uwezo wa kusambaza mbegu,utoaji huduma za umwagiliaji ,utafutaji wa masoko wa bidhaa za kilimo a mazao yake,kuwa na huduma bora za usimamizi wa mazao na uongezaji wa thamani na kuhamasisha mbinu za twknolojiabza kilimo.” amesema Kusaya.

Kuhusu majukumu katika mashirikiano hayo amesema ni kuanzisha utafiti wa pamoja ili kufikia kwenye kilimo biashara,kuanzisha mpango wa kuhamasisha usambazaji Teknolojia za kilimo na kubadilishana taarifa za upatikanaji wa masoko.

Awali Kaimu Mkuu Tawi la Utawala JKT Kanali Hassan Mabena amesema Jeshi hilo limeendelea kutekeleza shughuli za uzalishaji mali kwenye sekta ya kilimo ,mifugo na uvuvi ambapo utekelezajibwa shughuli hizo umelenga kuzalisha mazao ya chakula ili kufanikisha azma ya JKT ya kujitosheleza kwa chakula na kuipunguzia Serikali gharama za kulisha vijana wanaopata mafunzo katika makambi yao.