Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Mbeya
MKUU wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema siri ya mafanikio kwa Jeshi hilo katika uzalishaji wa mazao katika mashamba ya JKT ni mawasiliano yanayofanywa na Jeshi hilo kujua hali ya hewa ya kipindi husika.
Akimwakilisha Mkuu wa JKT katika maonyesho ya Nane Nane kwenye viwanja vya John mwakangale Jijini Mbeya, Brigedia Jenerali Mabena amesema,wamekuwa wakiwasiliana na Mamlaka ya Hali ya Hewa ili kujua hali ya mvua ya kipindi husika na kutaka kufahamu gani wanaweza kuanza shughuli ya kupanda mazao.
Amesema,hatua hiyo imefanya pamoja na mabadiliko ya tabianchi lakini bado katika vipando vya JKT na mashamba yake kwa ujumla yaliyopo vikosini kuendelea kufanya vizuri mazao yameweza kustawi kwa jinsi ambavyo walikuwa wametarajia.
“Siri ya mafanikio kwa JKT katika uzalishaji wa mazao katika mashamba yake ni kwamba sisi tulishaiona hiyo changamoto ya mabadiliko ya tabianchi,kwa hiyo tunachokifanya ni kuwasiliana na Mamlaka ya Hali ya Hewa ili kujua hali ya mabadiliko ya tabianchi hasa kwenye eneo la mvua,
“Kwa hiyo walikuwa wakituambia msimu huu mvua zitawahi au zitachelewa na hata kama zitawahi basi zitakuja kwa kiwango kidogo sana kwa hiyo baada ya kupata taarifa hiyo JKT tulikaa chini na kuweza kuona kwamba ni aina gani ya mbegu ambazo zitaendana na hali ya hewa iliyopo,lakini pia tuanze kulima mapema”amesema na kuongeza kuwa
“Mfano kikosi cha 847 Milundikwa,pale kikosini wamefanikiwa sana ,wameweza kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa sababu baada ya kuwasiliaana na mamlaka ya hali ya Hewa waliweza kulima mapema na kupanda mapenda na kutumia mbegu zenye uwezo wa kuhimili ukame.”
Vile vile Brigedia Jenerali amesema,JKT wanataka kuondoakana na kilimo cha kutegemea mvua,ambapo Jeshi hilo limekuja na kilimo mkakati wa umwagiliaji ambapo tumeanza kikosi 837 Chita tayari Skimu ya umwagiliaji imeshafikia zaidi ya asilimia 80 ya ekari 2500.
Amesema mpango uliopo ni kulima ekari 12,000 zilizopo kikosi cha Chita zote zinajengewa skimu ya umwagiliaji na hivyo JKT kuondokana na kutegemea mvua kwani watakuwa na uhakika wa wanachokilima na uhakika wa nini wanakwenda kuvuna.
Ametumia nafasi hiyo kuzungumzia mikakati yao katika kupambana na uhaba wa mafuta ya kula nchini ambapo amesema, JKT limejipanga kukabiliana na hali hiyo na kwamba , tayari wameshaanza kuboresha shamba la michikichi Kikosi 821 Kigoma.
“Sasa hivi tunalima na tunataka kuhakikisha kwamba tunaweza kupanda ekari 2,000 za michikichi ,na mwelekeo wetu ni kuhakikisha kwamba tunakuza lile shamba kwa hiyo tutapata mafuta kutokana na michikichi,
“Lakini pia kwa upande wa alizeti tuna vikosi vyetu vipo Dodoma karibia na Singida kule mikoa ya Iringa,Manyara,mkakati uliokuwepo ni kuja na mpango wa kuongeza mashamba hayo lakini zaidi tutawasiliana na wenzetu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) ili tuweze kupata wataalam wa mbegu wakishirikiana na wataalam wa JKT katika kupata mbegu bora zitakazotumika katika mashamba ya JKT na wakulima wengine waliopo Tanzania ambazo zitakwenda kutoa uhakika wa mazao mengi na hatimaye kuhakikisha tunakabiliana na uhaba wa mafuta.
More Stories
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari