December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

JKT ina uwezo kuwa ghala la chakula barani Afrika

Na Joyce Kasiki ,Tmesmajira online,Dodoma

MAKAMU wa Rais Dkt.Philip Mpango amezindua maonyesho ya wiki ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa(JKT)  huku akitoa rai kwa Jeshi hilo kuangalia namna ya kulifanya Taifa liwe ghala la chakula Barani Afrika.

Akizindua maonyesho hayo katika viwanja SUMAJKT Tower jijini Dodoma ,Dkt Mpango ametumia nafasi hiyo kulipongeza Jeshi hilo kwa shughuli mbalimbali inazofanya inazofanya za uzalishaji Mali ikiwemo  kwenye kilimo.

“JKT linaweza kuwa fursa ya kufanya nchi ya Tanzania kuwa ghala la chakula,naamini Jeshi hili lina uwezo wa kuwa chachu ya kuifanya Tanzania kuwa Ghala la Chakula,hivyo  naomba Uongozi wa JKT kubuni mbinu mpya za kuchagiza Agenda ya kuifanyaTanzania kuwa Ghala ya Chakula katika Ukanda Wa Bara la Africa na hata pande zingine za Dunia.”amesisitiza Dkt.Mpango

Aidha Dkt.Mpango ameliasa Jeshi hilo kuwekeza zaidi zatika zufundisha zijana zatumizi ya zeknolojia zatika zhughuli zake zbalimbali za uzalishaji Mali na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Pia amelitaka JKT liendelee kuunga mkono juhudi za Rais na serikali yake katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira ,upandaji miti , pamoja na utunzaji wa vya maji kwa ajili ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Dkt.Mpango ametumia nafasi hiyo kulipongeza JKT ,Matawi yake yote na Shirika lake la Uzalishaji Mali (SUMAJKT)kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana miaka 60  tangu kuanzishwa kwa JKT ,ambayo yanaonekana kuchangia katika  pato la Taifa kupitia shughuli mbalimbali za uzalishaji mali katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi ,biashara na viwanda.

Aidha, Mpango ametoa rai kwa wananchi wote wa Mkoa wa Dodoma na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi katika wiki nzima ya maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambayo imeanza leo Julai Mosi 2023 huku kilele cha maadhimisho hayo kikiwa ni Julai 10,2023.

Kwa Upande Wake  Waziri Wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Innocent Bashungwa amesema katika wiki hii ya JKT ,wananchi wataelezwa kwa kina shughuli za jeshi hilo katika maeneo mbalimbali hapa nchini huku akisema JKT litaendelea  kujenga uwezo katika kilimo mkakati ambacho kitachangia pato la Taifa lakini pia kuwawezesha vijana kujitegemea.

Aidha Waziri Bashungwa amesema Wizara yake n itaendelea kushirikiana na wizara za kisekta katika kuboresha Mafunzo ya Stadi za kazi Kwa vijana wa JKT na kuwawezesha kwa kuwapatia ujuzi na maarifa zaidi ya ilivyo sasa .

Awali Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema,tangu kuanzishwa kwa Jeshi hilo 1963 mpaka Sasa ,limeendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi kwa ufanisi mkubwa na kufanikiwa kubadili fkira za vijana kwa kwa kuwajenga katika hali ya umoja,moyo wa kupenda kazi ,uadilifu, nidhamu, uzalendo na Uelewano bila kubaguana kwa misingi ya Dira, Udini, jinsia na kudumisha uhuru na Amani ya Taifa.

Julai 10 mwaka huu Jeshi la Kujenga Taifa linatimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwake  Julai 10,1963.