December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

JK kuzindua albamu ya kwanza ya Ommy Dimpoz

Na Penina Malundo, timesmajira

RAIS Mstaafu, Jakaya Kikwete, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa albamu ya kwanza ya staa wa muziki nchini, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.

Uzinduzi wa albamu hiyo inayojulikana kwa jina la ‘Dedication’, utafanyika leo katika hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ommy Dimpoz, amesema albamu hiyo imebeba takribani nyimbo 15 na amewashirikisha wasanii mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Amesema katika uzinduzi huo amewaalika wanasiasa, mabalozi, wasanii na mawaziri ambapo baada ya uzinduzi kutakuwa na sherehe ambayo itafanyika katika ukumbi wa Element.

Dimpozi amesema albamu hiyo ameipa jina hilo kutokana na mengi aliyopitia wakati anatafuta maisha.

Nyota huyo amesema albamu hiyo tayari ipo katika mitandao yote na baadhi ya wasanii ambao amewashirikisha ni Marioo, Nandy, Fally Ipupa, Dj Kerozen, Blaq Diamond, Julio Masid na wengine.