December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

JK ashauri kupunguzwa bei za gesi,umeme

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online

RAIS Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete amesema vita dhidi ya nishati safi ya kupikia nchini itafanikiwa endapo gharama ya umeme na gesi zitapungua.

Dkt Kikwete ameyasema hayo alipotembelea banda la TANESCO kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam.

“Maadui wawili  wa mazingira yetu  ni kuni na mkaa,kwa hiyo kama napambana yataelekezwa katika kupunguza gharama za umeme na gesi itasaidia katika matumizi ya Nishati safi ya kupikia.”alisema Dkt.Kikwete na kuongeza kuwa 

Kwa mujibu wa Dkt.Kikwete,watu wengi nashindwa kuhusu gharama za gesi na umeme kwa ajili ya kupikia huku akisema kama gharama hizo zitakuwa kwa gharama.nafuu kama ilivyo kwa kuni na mkaa,basi vita dhidi ya Nishati safi yabkupikia unafanikiwa na hivyo kuokoa mazingira.

 Akiwa katika banda la Wakala wa Nishati  Vijijini(REA), Dkt.Kikwete baada ya kukagua majiko yanayotumia umeme aliishauri REA kuja na mpango utakaowasaidia watu wasiokuwa na uwezo kutumia nishati safi ya kupikia kwa gharama nafuu.

“Vitu mnavyovileta hapa kama Nishati nafanya kupikia ni kwa ajili ya watu wenye uwezo tu,Bali mnapaswa kuleta na vile vya gharama nafuu ambavyo kila mtu anaweza kuhusu gharama.” Amesisitiza