Na Mwandishi Wetu
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Masuala ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education) – GPE) yuko Seoul, Korea Kusini kwa ajili ya kukutana na viongozi wa serikali na mashirika mbalimbali ya Korea Kusini kwa ajili ya kujadili mikakati ya kuendelea kuboresha elimu katika nchi zinazoendelea. GPE ambayo ilianzishwa na nchi za G7 miaka 20 iliyopita, imeendelea kupigania elimu kwa ajili ya mtoto wa kike na wa kiume kwa kuomba kuungwa mkono na nchi na taasisi zinazoweza kuchangia katika elimu duniani.
Kikwete ameambatana na Charles Noth, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo yenye makazi yake Washington DC, Marekani.
Akiwa Seoul, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Park Yongmin, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini.
Aidha, amekutana na Lee Yunyoung, Kaimu Rais wa Shirika la Serikali ya Korea la Maendeleo Kimataifa (KOICA).
Kesho Mheshimiwa Rais Kikwete anatarajiwa kuzungumza na Wabunge wa Korea Kusini na kufanya mazungumzo na Mhe. Ju-ho Lee, Naibu Waziri Mkuu wa Korea Kusini
More Stories
Prof.Muhongo awapongeza vijana 32 waliotembea kwa miguu kutoka Butiama hadi Mwanza
Rais Samia atimiza ahadi Hanang
Daktari Dar ajishindia Mil. 100/- za Fainali NMB Bonge la Mpango