Na Aveline Kitomary,TimesMajira Online,Dar es Salaam.
UGONJWA wa shikizo la juu la damu (presha ya kupanda) hutokea wakati nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa ya moyo huwa kubwa kuliko kawaida .
Ongezeko hilo husababisha moyo kufanya kazi kupita kiasi ili kusukuma damu katika mishipa ya damu .
Kwa kawaida ugonjwa wa presha hauna dalili ili ukidumu kwa muda mrefu bila ya tiba kuna madhara makubwa kiafya .
Asilimia 95 ya wagonjwa wa presha ya kupanda hawana sababu zinazojulikana kisayansi .
Mara nyingi sababu zinazoainishwa ni historia ya ugonjwa katika familia ,uzito mkubwa ,matumizi ya chumvi nyingi,kutokufanya mazoezi ,uvutaji sigara ,ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi na umri mkubwa.
Asilimia ya watu wanaopata ugonjwa presha ya kupanda huwa wanakuwa katika kundi la magonjwa mbalimbali kama figo,mishipa ya moyo na mfumo wa homoni.
HALI ILIVYO
Katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) tangu ilipoanzishwa Septemba 2015 hadi Aprili 2020 kati ya wagonjwa 334,774 waliotibiwa asilimia 66 ya wagonjwa walikuwa na tatizo la presha ya kupanda.
Ripoti ya JKCI inasema tatizo la linaongezeka kulingana na mabadiliko ya maisha ya watu ikiwa ni pamoja na mfumo wa ulaji na kazi.
Daktari Bingwa wa Moyo, Samwel Rweyemamu anasema katika tathimini kwa maeneo ya mjini na vijijini kunaongezeko la asilimia 30 na 35.
“ Lakini inategenmea na mahali mfano nilifanya utafiti Songea nilivyofanya tathimini wale watu waliopima takribani 800 asilimia 64 walikuwa na shikizo la damu.
“Lakini pia hata Dar es Salaam shinikizo la damu linakaribia kwenye asilimia 40 mfano JKCI tangu tumeanza ukiangalia asilimia 70 ni wagonjwa wanakuja wakiwa na shinikizo la damu tatizo ni kubwa linaongezeka kila mwaka,”anabainisha Dk Rweyemamu.
AINA ZA PRESHA
Dk Rweyemamu anasema wakipima shikizo la juu la damu huwa wanaangalia rekodi mbili ambazo ni systolic na diastolic.
“Sistolic ikiwa iko sawa sawa na 140 au zaidi ni hatari na diastolic ikiwa 90 au zaidi tunasema huyu mgonjwa anatatizo la shinikizo la damu.
“ Shinikizo la damu limegawanyika katika sehemu mbili kuna inayoitwa primary high pertation au visababishi halisi havijajulika lakini tunaangalia viashiria.
“Lakini aina ya pili tunaiita secondary high pertation ambayo inaweza kusababishwa na magonjwa mengine hapa mtu anapata presha kwasababu kuna magonjwa mengine ndani yake.
VISABABISHI
Anasema viashiria vya hatari moja wapo uvutaji sigara,unywaji pombe kupindukia ,chakula hatarishi mfano kula chakula chenye chumvi nyingi au kuongeza chumvi kwenye chakula ,mafuta mengi.
“Inaweza kusababishwa na ulaji wa vitu vingi ambavyo ni hatari kwa afya mfano kuna vinywaji vyenye sukari nyingi kama soda, watu wanakula sana lambalamba kila gari ikipita watu wanalamba lamba vitu vyenye sukari mwisho siku itakuongezea uzito ulipindukia kwahiyo kutumia sukari ni mmoja wapo.
“Lakini pia kushindwa kufanya mazoezi (sedentary life) wataalamu wanapendekeza angalau kufanya mazoezi mara tatu kwa wiki ,kwa nusu saa unaweza kukimbia au kutembea,”anasema.
Anasema sababu nyingine ni ugonjwa wa figo kwani mtu akiwa na shida ya figo presha yake hupanda na akiwa na shinikizo la damu pia anaweza kupata ugonjwa wa figo.
“ lakini wengine wanaweza kuwa na kansa ya tumboni mfano adrenal gland kansa inasababisha na pia tezi la kwenye shingo ikiwa inatoa vichocheo kwa wingi inakusababisha presha,”anabainisha.
HUATHIRI NGUVU ZA KIUME
Dk Rweyemamu anasema tatizo la shinikizo la juu la damu linaweza kuathiri nguvu za kiume.
“kwa wanaume zaidi sahivi kuna tataizo la nguvu za kiume unakuta wengi wanakuja wanakuambia huko nyumbani familia inalalamika kwasababu ya shinikizo la damu lakini pia kwasababu ya madawa mengine yanasababisha ukosefu wa nguvu za kiume.
“ Hili ni shida inayojitokeza ni jambo linaoneka kama watu wanashindwa kulieleza vizuri lakini watu walio wengi wanakuja,Hatujawahi kufanya na utafiti wa kuona tatizo hilo lipo kubwa kias gani lakini lipo,”anafafanua.
Anasema Wanaume wanaougua shinikizo la juu la damu wako hatarini kupungukiwa nguvu za kiume.
Dk Rweyemamu anaainisha madahara mengine kuwa ni moyo kuharibika ,kupata kiharusi ,figo zitaharibka,macho yataharibika.
WAGONJWA HUATHIRIKA SAIKOLOJI
Dk Rweyemamu anasema kuna uwezekanao wa wagonjwa kuweza kupata tatizo la kisaikolojia kulingana na mapokeo yao.
“Nilikuwa na mgonjwa ambaye niliambiwa mwezi uliopita haongei lakin kwa sasa anasema kuwa anaona watu usiku mpaka leo hajalala kwenye familia.
“hizo ni dalili za awali za kujua kuwa mgonjwa huyu sasa alikuwa na presha na mishipa ya moyo ikaziba na akafanyiwa oparationa hali hiyo inamfanya anaanza kupata sonona (depression).
“ Sasa anaelekea kupata magonjwa ya akili kwahiyo tunaona alianaza na presha mishipa ya damu ikazaiba amefaniyiwa upasuaji sasa anaenda kupata sonona.
Anasema jinsi ya kuwasaidia watu wenye tatizo hilo ni kuwapeleka kwa mwanasaikolojia ili kupewa ushauri.
“Tunaangali jinsi ya kumsaidia kwa kumpeleka kwa msaikolojia anaweza kuta msaada, Tukiona mtu anaumuhimu wa kuhitaji saikolojia tunampeleka,”anaeleza.
UELEWA BADO MDOGO
Dk Rweyemamu anasema utafiti uliofanyka Simanjiro Mkoani Manyara na Kisiwa cha Mafia kiasi cha uelewa ulikuwa chini ya asilimia 50.
“ lakini tunatoa huduma ili watu wapate mwamko lakini unakuta watu walio wengi wanashikizo la damu lakini hawaelewi kama wanashikio la damu.
NJIA YA KUEPUKA
Mfumo bora wa maisha unatajwa kuwa na nafasi kubwa zaidi katika kuepuka magonjwa hasa magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Dk Rweyemamu anataja mfumo bora wa maisha kuwa suluhisho namba moja ya kuweza kuepuka na presha na magonjwa moyo.
Anasema aina ya ulaji wa vyakula na jinsi ya ufanyaji mazoezi au kazi hufanya mwili kuwa katika hali ya kukabili magonjwa au kuepuka kabisa.
“Kuna aina ya vyakula na vinywaji mtu anatakiwa kuviepuka mfano kunywa juisi kila wakati ,pipi na vitu vingine vyenye sukari, kupunguza chumvi hivi ni muhimu sana kitabibu,na kingine mtu kupunguza uzito kama ni mkubwa kwasababu unaweza kutumia dawa za presha lakini kama wewe unakilo 150 hata nikikupa dawa za presha zikaisha zote kurudi kawaida inakuwa ni vigimu sana.
Anasema ni lazima kuweka uwiano mzuri wa afya ya mwili kutokana na dawa za presha siku zote ambazo mgonjwa ataishi
“Kwanza dawa za presha au moyo hazikai mwilini au tumboni zikishatumika zinatoka kwa njia ya mkojo kwahiyo mgonjwa anatakiwa kutumia dawa kila siku.
“Matumizi ya dawa za presha na moyo yataisha pale ambaapo uhai wa muhusika utafika mwisho hapa Duniani.
“Wakati mwingine tunachokifanya presha ikishuka tunapunguza dozi au kuondoa baadhi ya dawa ili mgonjwa apate dawa inayoendana na presha yake hivyo kazi yetu ni kurekebisha tu na sio mgonjwa kuacha kutumia dawa kabisa,”anaeleza Dk Rweyemamu.
LISHE KWA WAGONJWA
Husna Faraji ni Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI)anasema kuwa katika lishe wanatazama mambo mbalimbali ambayo wanaweza kubaini kama muhusika analishe bora.
“Tunahitaji jamii ielewe kuwa tunapozungumzia ulaji usiofaa ni kutokuzingia makundi ya chakula na kiasi cha makundi ya chakula, tunasisitiza aina ya makundi ya chakula iliyopo lakini kingine ni kula makundi ya chakula kwa kuzingatia uwiano uliosahihi.
“Ulaji wa mboga za majani ni muhimu zaidi kutokana na faida nyingi za kiafya zinazopatikana lakini tunashauri kiwango cha mafuta na aina ya mafuta yanayotumika katika vyakula.
“Ushauri ni kuwa ni bora watu wakatumia mafuta ya mimea badala ya wanyama,hii ni kwasababu mafuta yanayotokana na wanyama yana ‘cholesterol’ mbaya ambazo zinahusishwa na matatizo ya moyo kwani huziba mishipa ya damu kwenye moyo hivyo kuongeza nafasi ya kuweza kupata presha ya kupanda,”anafafanua.
Husna anasema matumizi ya vyakula vinayosindikwa viwandani ni hatari moja wapo kwa mtu kupata presha na magonjwa ya moyo.
“Matumizi ya vinywaji kama soda ambazo utayarishaji wake huwa unaviwango vikubwa vya sukari hii hupelekea shida katika afya ya moyo, tunashauri watu kupendelea vinywaji yenye virutubisho zaidi kama maziwa ,juisi ya matunda ,maji safi na salama kuliko kutumia viwanywaji amabavyo vinasindikwa kwa muda mrefu kwa sukari na chemikali,”aanasema Husna.
Anasisitiza watu kupunguza ulaji wa vyakula yenye wanga kutokana na aina hivyo ya vyakula kuweza kusababisha matatizo ya moyo
“Wanga inaongeza uzito hali hiyo inaongeza nafasi ya kupata presha ya juu na matatizo ya moyo magonjwa mengine yasiyo ya kuambukizwa kama kisukari kansa na mengineyo.
“Lakini pia tunasisitiza ufanyaji wa mazoezi kwasababu mtu anayefanya mazoezi tafiti zinaonesha huwa na uwezo wa kupunguza nafasi ya kupata magonjwa hivyo nashauri hasa tunapokuwa na uzito uliokithiri tuwe na ratiba ya mazoezi kila siku,”anashauri Husna.
Mwishooooo…..
More Stories
Boost ilivyoboresha miundombinu ya elimu Ilemela
Samia apongeza walimu 5,000 kupatiwa mitungi ya gesi, majiko kutoka Oryx
Uwekezaji kwenye kilimo utatimiza ndoto ya Samia ya nchi kuwa ghala la chakula Afrika