Na Mwandishi wetu,TimesmajiraOnline,Dodoma
CHAMA Cha Walimu Tanzania (CWT) katika Mkutano mkuu wa uchaguzi wa walimu wanawake na walimu wenye ulemavu wamekabidhi tuzo ya heshima kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kutambua mchango wao katika kudhibiti matukio ya uhalifu kwa watu wenye walemavu na jamii.
Hayo yamejiri leo,Juni 5,2025 katika mkutano huo ambao umehudhuriwa na walimu kutoka katika mikoa mbali mbali hapa nchini unao enda sambamba na kufanya uchaguzi wa viongozi.

Akizungumza katika mkutano huo Mara baada ya kupokea Tuzo hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi amesema tuzo hiyo ni heshima na italeta tija katika utendaji kazi katika kudhibiti matukio ya uhalifu katika mkoa wa Dodoma hususani watu wenye ulemavu.
Aidha Katabazi amasema Jeshi la Polisi litahakikisha ulinzi na usalama unatamalaki katika maeneo yote, yeyote atakae jaribu kufanya uhalifu hususani kwa watu wenye ulemavu atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
“Jeshi la Polisi ni rafiki wa wote kwa wale ambao wanategemea kufanya uhalifu au kuwadhuru walemavu kutokana na changamoto walizo nazo hatuta sita kuwachukulia hatua stahiki kwa mujibu wa sheria, fanyeni uchaguzi wa haki na niwakikishie mpo katika mikono salama ya Jeshi la Polisi” Amesema (SACP), katabazi.



Vilevile, Katabazi amewaasa walimu kuendelea kushirikiana na kuliamini Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu pindi wanapo kuwa wanatekeleza majukumu yao majumbani na mashuleni.
Kwa upande wao uongozi wa Chama hicho umeeleza sababu ya kutoa tuzo hiyo ni pamoja na ushirikiano ulikuwepo baina ya Jeshi la Polisi wananchi,walimu na walemavu kwa kuimarisha ulinzi pamoja na kuwakumbuka watu wenye uhitaji.
Mgeni rasmi katika ufunguzi huo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe, Ummy Nderiananga.
More Stories
TFS yawakaribisha wawekezaji katika vivutio vya utalii wa misitu
Waziri Bashungwa:Tumieni teknolojia za kisasa kudhibiti uhalifu unaovuka mipaka
Flightlink kuzindua Safari za Ndege za Kila Siku kwenda Nairobi wiki ijayo