December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jeshi la Polisi latakiwa kuwekeza kwenye Teknolojia ili kupambana na uhalifu kisasa

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.

WIZARA ya Habari Mawasiliano na Teknoljia ya Habari imelitaka Jeshi la polisi Nchini liamue kuwekeza kwenye Teknolojia ili kurahisisha utendaji kazi wao katika kupambana na uhalifu wa mtandao.

Hayo yamesemwa jijini hapa leo na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhandisi, Andrew Kundo wakati akifungua mafunzo ya Makosa ya mtandao (CYBERCRIME)kwa wapelelezi na askari wa chumba cha mashtaka(CRO) ambapo alisema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza
ujuzi namna ya kukabilina uhalifu wa kimtandao.

“Mafunzo haya ni ya muhimu kwa Dunia ya leo ambayo imejawa na uhalifu kwasababu ya ongezeko la wabuni mbinu za uhalifu ni wengi  na kila siku wanabuni mbinu mpya za uhalifu hivyo ni vyema kujua zaidi jinsi ya kukabiliana nao,”amesema.

Amesema Kamati ya mafunzo hayo pamoja na mambo mengine ilipendekeza kwa Serikali kutoa mafunzo hayo na  serikali iliridhia mafunzo hayo ili kumfanya askari kuwa bora kwa sababu mhalifu anaweza kuwa bora lakini askari anatakiwa kuwa bora zaidi ili kuweza kukomesha uhalifu huo.

“Lakini mkishapata mafunzo haya mzingatie ili kuhakikisha tunaenda kuboresha matumizi ya teknolojia katika jeshi la polisi lazima tutumie vyombo vya habari kuelimisha wananchi kuhusu matumizi sahihi ya mitandao watambue nini maana ya kosa la mtandao na kipengele kipi nikifanya inakuwa kosa la kimtandao,”amesema.

Pamoja na hayo amesema lengo la jeshi la polisi ni kuwa la kisasa na linalojibu kiu ya watu katika utekelezaji wa huduma bora ndio maana Mafunzo hayo yanafanyika Morogoro,Dar es Salaam na Dodoma.

“Wakufunzi hawa wanajua kinachoendelea hivyo wako vizuri na wanajua nini wawapatie ili mtoke kwenye mafunzo mkiwa mnafahamu nini chakufanya ili kukomeshq uhalifu wa kimtandao kwa kutumia teknolojia za kisasa,”amesema.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa mashtaka nchini (DCI),kamishna msaidizi mwandamizi  wa polisi(SACP)Deusdedit Nsimeki,amesema mafunzo hayo kupata uelewa mpana wa sheria ya makosa ya mtandao na kufanya taaluma hiyo katika kumsaidia mwananchi sio kujipatia kipato.

Amesema kumekuwa na malalamiko toka kwa baadhi ya wananchi ambao wamekuwa na kesi ya kupotelewa na simu zao kulipia gharama kubwa tofauti na simu ambayo imepotea na hivyo kuharibu taswira ya jeshi na taaluma kwa ujumla.

“Mafunzo hayo yatasaidia kuongeza tija na uadilifu katika utendaji kazi wenu ikiwa ninpamoja na kupambana na uhalifu na kupelekea kufanyakazi kwa ushirikiano mkubwa,”amesema.

Kwa upande wake Kamishna wa Polisi uchunguzi wa kisayansi (CP)Shabani Hiki,amesema wao kama MA CRO ni kama msingi katika nyumba kwani taswira ya jeshi la polisi ipo kwao hivyo  jukumu lao ni kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa kwa kupunguza malalamiko.

Amesema Kama watafanya kazi vizuri watasaidia kuondoa malalamiko toka kwa wananchi wale ambao huenda kwajili yakupata huduma katika masuala ya mashtaka.