Na Mwandishi wetu,Timesmajira
MUIGIZAJI Jesca Mtoi ameibuka kidedea katika tuzo ya mwingizaji bora wa Kike,katika Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) lililofanyika hivi karibuni.
Filamu iliyompatia ushindi Jesca,The MidnightBride ni filamu ambayo imempatia umaarufu katika kipindi kifupi cha uigizaji wake ambapo amevaa uhusika na kuvutia watu wengi zaidi.
Akizungumza hayo mara baada ya kupokea Tuzo ya ZIFF hivi karibuni,amesema tuzo aliyoipata ni ya muigizaji bora wa Kike Tanzania ambayo imempa faraja kubwa katika kazi zake za sanaa.
”Tuzo hii imenipa faraja kubwa inaonesha nilipoanza ni pazuri na imenipa motisha ya kujifunza na kufanya bora zaidi ya kupata kazi nyingine,”amesema na kuongeza
”Sikuwa nategemea lakini namshukuru Mungu kupewa nafasi ya heshima hii,natumaini nitafanya vizuri zaidi kwa kazi zijazo.
Amesisitiza kuwa hii ni kazi yake ya kwanza kufanya na imemfikisha mahali pakubwa hivyo mashabiki zake watarajie makubwa kutoka kwake.
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam