Na Penina Malundo, TimesMajira Online
JAMII imetakiwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na watu kwenye ulemavu hususani katika sekta ya michezo ili nao waweze kutumia fursa mbalimbali za michezo.
Wito huo umetolewa na Mratibu wa Masoko na Matukio kampuni ya Image consultation, Martha Kambo baada ya kumalizika kwa michuano ya Mpira wa kikapu kwa timu za watu wenye ulemavu, iliyoyanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Don Bosco, Oysterbay.
Katika michuano hiyo ambayo ilishirikisha timu nne za Pangani na Azania kwa upande na wanaume na Overland na Image kwa wanawake, mgeni rasmi alikuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha aliyewakilishwa na Milinde Mahona huku Winston Thomas akiibuka MVP kwa wanaume na kwa wanawake MVP alikuwa Ashura Sadiki.
Winston pia alikuwa mchezaji aliyefunga pointi nyingi kwenye michuano hiyo wakati Mwajabu Athumani akiibuka kinara kwa upande wa wanawake.
Martha amesema kuwa, dhumuni ya kufanya tamasha hilo lilikuwa ni kuwakutanisha watu hao wenye ulemavu wanaocheza mpira wa kikapu lakini pia kuikumbuka jamii watu hao ambao nao wana umuhimu mkubwa ndani ya jamii.
Kutokana na kampuni yao kujishughulisha na matukio mbalimbali yanayofanywa na watu mbalimbali, waliona ni vema kurudisha faida kwa wananchi hasa kundi hilo ambalo mara zote limekuwa likiachwa nyuma.
“Tasnia ya michezo kwa walemavu kidogo katika jamii yetu haijawekewa nguvu sana hivyo tuliona hii ni nafasi ya mwanzo wa kuionyesha Tanzania kuwa ni sekta inayotakiwa kuangaliwa kwa umakini kwani watu wenye ulemavu wanahitaji kuwasaidia na kuinuliwa kimichezo,”.
“Wote mmeona viwango vya timu zilizochuana leo ambazo pia zipo zilizokwenda hadi nchini Kenya kushiriki mashindano na kufanikiwa kuwa washindi watatu hivyo hawa watu ni muhimu sana katika michezo yetu Tanzania na wanaweza kufika mbali zaidi ikiwa tutawapa ushirikiano wa kutosha ,” amesema Mratibu huyo.
Kwa Upande wake Mshindi wa tatu wa Miss Tanzania, Priscon Lyimo amesema kuwa, michezo kwa watu wenye ulemevu ni mizuri kwani inawapa fursa ya kujitanua na kujiona na wao wapo kama walivyo watu wengine wanaoweza kushiriki michezo.
Amesema, ni vema sasa watu wakajitokeza kwa wingi na kuwainua watu hao kwani wakiwezeshwa wanaweza kufika mbali zaidi na kupata fursa mbalimbali kupitia michezo .
Afisa Rasilimali Watu na Utawala wa Kampuni ya Lake Group, Wilfred Massano, amesema wakiwa kama miongoni mwa wadhamini wa shindano hilo wamekuwa wakijitokeza kuwainua watu hao katika masuala ya michezo kwani na wao wana wana ndoto zao katika michezo ambazo ili kuzifikia ni lazima wasaidiwe kikamilifu na wadau mbalimbali.
More Stories
Watumishi wa Fahari wafanya Bonanza
Rais Samia atia mkono mchezo wa masumbwi Tanzania
Chino bingwa mpya wa IBA Intercontinental Championship