November 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kaimu Meneja wa Bodi ya Nyama(TMB)Dkt. Imani Sichalwe akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya kimataifa Sabasaba yanayofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es salaam Picha na Irene Clemence

Jamii yashauriwa kula nyama kwa wingi

Na Irene Clemence, TimesMajira Online, Dar es Salaam

JAMII imeishauriwa kujenga mazoea ya kula nyama kwa wingi kwani husaidia kuleta vichocheo katika mwili wa binadamu.

Akizungumza na waandshi wa habari jijini Dar es salaam katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba, Kaimu Meneja wa Bodi ya Nyama(TMB) Dkt. Imani Sichalwe amesema, ulaji wa nyama usaidia kuchochea homoni za mwili hivyo
kila mtu anatakiwa kula nyama kilo 50 kwa mwaka ili kujenga afya bora na kupata protini kwa wingi.

Amesema, ulaji wa nyama ni muhimu katika mwili wa binadamu kwasababu usaidia kutengeneza mifupa, ujenzi wa akili pamoja na kuongeza homoni mwilini.

“Ulaji wa nyama unaokidhi viwango uisaidia jamii kujenga mwili na kuongeza homoni za kutosha na kuondoka na tatizo la magonjwa mbalimbali ikiwamo ukosefu wa uzazi,” amesema Dkt. Sichwale.

Alisisitiza kuwa watu ambao awali nyama wamekuwa wakikosa vitu vingi katika mwili wao jambo ambalo uchangia kupungu kwa protini zao.

“Ubora wa protini ulioko katika nyama ni mkubwa zaidi kuliko ubora mwingine ambao unakosekana katika protini nyingine,”amesema Dkt Sichwale.

Akizungumzia Maonesho ya Sabasaba, Dkt. Sichwale amesema wamekuwa wakionesha kazi mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na bodi hiyo ikiwemo kutoa mafunzo katika mmyololo mzima wa thamani ya nyama.

“Tukizungumzia suala la nyama linatakiwa lianzie katika mashamba ambako kuna uchaguzi wa mbegu, ulishaji mifungo pamoja na usafirishaji,” amesema Dkt. Sishwale.

Aidha amesema, wamekuwa wakiamasisha wananchi juu ya ujenzi wa Viwanda vya kisasa ikiwemo machinjio pamoja na kujua namna ya kusafirisha vyema mifungo na nyama.