November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jamiı yahimizwa kuwatumia maofisa maendeleo kwenye miradi

Na Queen Lema, Timesmajira Online,Arusha

Wataalamu wa sekta mbalimbali hapa nchini wameaswa kuhakikisha kuwa kila kazi pamoja na miradi ambayo wanaipitisha ndani ya jamii wahakikishe kuwa wanawatumia maafisa maendeleo kwani wao wana uwezo wa kutambua mahitaji maalumu ndani ya jamii.

Kwani sasa wapo wataalamu,wadau wa maendeleo ambao wanatekeleza miradi yenye thamani kubwa lakini haiwasaidii.

Hayo yameelezwa katika chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru na Profesa George Kinyashi wakati wa mhadhara wake wa kwanza wa kiprofesa uliokuwa unahusu maendeleo yanayoongozwa kisekta hapa nchini.

Profesa George amesema kuwa ndani ya jamii ipo miradi mingi ya maendeleo ambayo inafanywa kwa gharama kubwa lakini inashindwa kuwa sehemu ya faida kwa jamii kutokana na kukosekana kwa ushauri kutoka kwa Maofisa Maendeleo.

Ameongeza kuwa Maofisa Maendeleo ya Jamii wana nafasi kubwa sana hasa katika kuleta mapinduzi ya kisekta endapo tu kama watashirikishwa kwenye mipango.

“ifike mahali sasa jamii ione umuhimu wa kuwashriikisha hawa Maofisa Maendeleo ya Jamii kwa kuwa wao ni rahisi kujua nini kinahitajika na kundi lipi linahitaji mradi gani na kwa wakati gani,”.

Katika Hatua nyingine amewataka Maofisa Maendeleo ya Jamii kuhakikisha kuwa wanaachana na dhana ya kuridhika na kiwango cha elimu walichonacho na badala yake kila mara waongeze elimu ambapo kwa kufanya hivyo kutaweza kuwasaidia kuongeza idadi ya miradi kwenye jamii.