Na Penina Malundo
JAMII inatakiwa kuendelea kuwa na uelewa wa utunzaji wa Udongo nchini ambapo asilimia kubwa ya udongo huo umekuwa unasaidia uzalishaji wa chakula kwa asilimia 95.
Akizungumza katika leo katika zoezi la kutembea umbali wa Kilometa tano kwaajili ya kuadhimisha siku udongo duniani,Balozi wa India nchini Tanzania ,Binaya Pradhan amesema maadhimisho hayo yanatoa uelewa kwa jamii kwa kuona ni namna gani udongo unatakiwa kutunzwa kwani ni sehemu mojawapo ya uzalishaji wa Chakula.
Amesema kuna madhara makubwa kama udongo ukitumiwa vibaya ikiwemo kusababisha uhaba wa Chakula,Shida ya Maji na Upotezaji wa Bioanuwai .
“Katika bara la Afrika asilimia 65 ya ardhi yenye rutuba tayari imeharibiwa na kuathiri watu milioni 485 hivyo tunaweza kuchukua hatua na kugeuza hili na kutekeleza angalau asilimia 3 hadi 6 ya maudhui ya kaboni ya jwenye udongo au Chakula cha Udongo,”alisema
Alisema matembezi hayo yanalengo la kuendesha sera ya kitaifa kwa kuongeza uelewa ba kuhamasisha watu wa watanzania kuunga mkono maamuzi hayo yanayozingatia mazingira.
“Udongo sio mali yetu ni urithi ambao tumeupokea kutoka kwa vizazi na ni jukumu letu kuhakikisha maisha ya udongo yanakuwa marefu na kujikimu kwa vizazi vijavyo,”amesema
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato