Na Patrick Mabula , Shinyanga.
Mratibu wa mahusiano ya jamii katika ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta EACOP mkoa wa Shinyanga, Cecilia Nzeganije ameitaka jamii kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazopatika katika ujenzi wa mradi huo toka Uganda hadi Tanzania.
Akiongea katika warsha ya siku moja kwa wanachama wa klabu ya Waandishi wa habari wa mkoa Shinyanga ( SPC) kuhusu utekelezaji wa mradi huo alisema wananchi hawajajitokeza kikamilifu kuchangamkia fursa tenda mbalimbali za kiuchumi zinazotangazwa kwenye mradi huo.
Nzeganija amesema katika ujenzi wa mradi huo wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda kwenda Chogorogeni mkoani Tanga linapita katika mikoa nane hapa nchi na moja ya utaratibu pale linapopita wananchi wa eneo husika waweze kunufaika kiuchumi kwa tenda mbalimbali zinohitajika.
Amesema kuwa wamekuwa wakitangaza tenda za fursa mbalimbali za kiuchumi zikiwemo za kuhudumia kwenye ujenzi huo lakini wafanyabiashara na wajasiriamali wamekuwa wakisuasua kujitokea na kuwaomba wachangamkie tenda hizo.
Nzeganija ametoa wito kwa wafanyabishara na wajasiliamali pamoja na jamii kuchangamkia fursa hizo za kutoa huduma mbalimbali zikiwemo za kufanyakazi za vibarua nazile za kudumu kwa mjibu wa matakwa na utaratibu katika mradi huo.
Mkuu wa kitengo cha mahusiano na mawasiliano wa shirika la mafuta Tanzania TPDC , Marie Msellemu amesema jumla ya watu zaidi ya 4000 wameshapata ajila rasmi na zisizorasmi na kuwata watu kuchangamkia furasa zinazotangazwa katika maeneo ya mikoa 8 linakopita .
Mmoja wa maafisa katika mradi huo , Asiadi Mrutu alipokuwa akiwasilisha taarifa yake alisema ujenzi wa mradi wa bomba hilo la mafuta ghafi toka Uganda kwenda hadi mkoani Tanga unaendelea vizuri kwa kasi na zaidi ya watanzania20,000 wameomba kupata ajira za kudumu.
Afisa fursa kwa wazawa wa EACOP , Maryam Madia amesema mradi huo utaimalisha mahusiano katika ya pande zote mbili za nchi kwa upande wa Tanzania jumla ya wananchi 9,815 walisaini kupisha mradi na wameshalipwa fidia kwa asilimia 100 kati yao 339 wamejengewa nyumba za kisasa baada ya kupisha mradi huo.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini