Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Jambojet, kampuni ya ndege inayoongoza barani afrika kwa kuwa na viwango vya nauli vilivyo rafiki kiuchumi, imekuja Zanzibar kuwekeza kwenye sekta ya anga kati ya Kenya na Zanzibar ikitarajia kuanzisha safari za moja kwa moja kati ya Zanzibar na Mombasa kuanzia tarehe moja julai mwaka wa 2024.
Safari za ndege za moja kwa moja hadi Mombasa zinalenga kuongeza utalii na biashara kati ya Zanzibar na Mombasa. Hili linatarajiwa kuimarisha utalii na viungo vya usafiri, na kuongeza uwekezaji utakao dumisha utajiri wa kitamaduni, kidini, urithi wa kihistoria na rasilimali za uchumi wa buluu kati ya visiwa hivyo viwili.
Zanzibar inakuwa kisiwa cha kwanza barani Afrika ambapo shirika la ndege la jambojet linafanya safari za moja kwa moja, kutoka Kenya alisema Karanja Ndegwa, Mkurugenzi mkuu wa JamboJet. Safari za ndege za moja kwa moja kati ya Zanzibar na Mombasa zitapunguza gharama za usafiri wa anga kati ya visiwa hivi wiwili kwani nauli za Jambojet zinaanzia laki tano na themanini na tisa elfu (kwenda na kurudi) huku nauli za watoa huduma wengine zikianzia laki saba sitini na tisa elfu (kwenda na kurudi).
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano, na Uchukuzi, Dr. Khalid Salum Mohamed, aliwakaribisha ndege ya jambojet na kusema kuwa shirika hilo la ndege litaongeza idadi ya wasafiri wa kimataifa kuja Zanzibar, wengi wao wakiwa watalii na wasafiri wa biashara. “Kwa kuzingatia Dira ya Zanzibar ya 2050 ya kuongeza uchumi wa buluu na idadi ya wageni wanao tembea Tanzania, upanuzi wa kimataifa ni muhimu kusaidia kufikia lengo hilo,” alisema Waziri Dr. Mohamed.
“Urithi na utajiri wa Zanzibar umekuwa ukiwavutia wasafiri kutoka Kenya na kwingineko barani Afrika, wengi wao wakiwa watalii wanaopendelea visiwa visafi na urithi wa mji mkongwe.” Alisema Karanja “Shirika la ndege linaendelea kufanya kazi ili kufikia maeneo mapya na kuboresha uzoefu wa wageni,” aliongeza.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi