January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jaji wa mahakama kuu kanda ya Tanga akubali kuondolewa nyongeza ya madai na nyaraka

Na Hadija Bagasha Tanga,

Jaji wa mahakama kuu kanda ya Tanga,Fahamu Mtuliya amekubali kuondolewa nyongeza ya madai pamoja na nyaraka zote za bodi ya wadhamini wa taasisi ya Answaar Muslim dhidi ya Abdulah Mohamed na Nuriya Mohamed wanaoshitakiwa na taassi hiyo.

Hatua ya kuondolewa kwa madai hayo pamoja na nyaraka zote za bodi ya wazamini wa taasisi ya Answaar Muslim inatokana na Jaji Mtulya kuridhiwa na mapingamizi yaliyotolewa mahakamani hapo na upande wa wadaiwa kwenye shauri hilo.

Shauri hilo la Ardhi namba 3 la mwaka 2021, bodi ya wadhamini wa taasisi ya Answaar Muslim,inadai kuwa Abdulah Mohamed na Nuria Ahamed kama msimamizi wa mirathi ya Saidi Ahmed wamevamia Hospitali ya Shifaa iliyopo barabara ya 18 mjini Tanga.

Katika shauri hilo,jaji amepanga kusilikiza mapingamizi ya awali kwa maandishi kuwezesha upande wa mdaiwa kupeleka maelezo yao, kwa yale mapingamizi yaliyowekwa ya msingi.

Kesi hiyo itatajwa tena March 10 2022.