November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jaji mkuu Prof.Juma awataka majaji kutoogopa

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira online,Tanga

JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahimu Juma amewataka majaji wa mahakama ya Rufaa na Mahakama kuu kutoogopa kusema au kutoa taarifa katika vyombo husika wanapobaini mapungufu katika sheria.

Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar wanaoshiriki katika Mafunzo elekezi yanayoendelea katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.

Akifungua Mafunzo Elekezi kwa Majaji 31 wa Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuuu Tanzania Bara na Visiwani ambao waliteuliwa na kuapishwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Juma pia amewataka majaji kuzingatia maadili na uadilifu na kuweka Mungu mbele katika maamuzi yao kwa sababu maamuzi hayo yanagusa maisha ya watu wengi..

Baadhi ya Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu ya Zanzibar wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma wakati wa uzinduzi wa Mfunzo elekezi.

Amesisitiza juu ya jukumu kwa majaji kuwa watafsiri wakuu wa sheria alisema kuwa wanapokwenda kufanya kazi watakutana na mapungufu ya sheria.

“Kazi kubwa ya majaji ni kutafsiri sheria na Katiba. Tafsiri zetu za sheria na katiba.

Profesa Juma amesema kuwa Majaji wajielewe kuwa wao ni viongozi na sehemu ya maboresho hivyo wasikae kimya wanabaini mapungufu katika sheria ili zinfanyiwe maboresho kwa faida ya watanzania.

Amesema kuwa Katiba imewakopesha viongizi hao wa Mmahakama mambo Fulani na kubakisha mambo mengine ambayo ni haki za wananchi zinatokiwa kulindwa zielekezwe katika ustawi wa watu. Katika Kila jalada utakalotolea hukumu unagusa maisha ya watu,”amesema Jaji Mkuu na kusisitiza umuhimu mkubwa wa majaji kufuata maadili na kuwa waadilifu.

Jaji Kiongozi wa Makama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akizungumza na Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu ya Zanzibar ambao hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa Mafunzo elekezi.

Amesema watu wengi wanasema sheria zibadilishwe lakini ukweli ni kuwa sheria nyngi si mbaya bali wakati mwingine binafsi za watu ndio zenye matatizo.

Amewataka majaji kuwa na tabia chanya na kwamba wananchi wana matarajio mengi juu yao kuhusu ulinzi wa haki zao..

Naye Jaji Kiongozi, Eliezer Feleshi alisea kuwa mafunzo hayo niya pili kufayika kwa Majaji Rufaa, ya sita kwa Majaji Mhakama Kuuu na mara ya Pili kwa majaji kutoka Tanzania Zanzibar.

Amesema kuwa mafuzo hayoyaaakisi sera ya mafunzo ya Mahakama na ni uthibitisho kuwa maboresho yanajengewa misingi bora ya utekelezaji.

Pia amesema kuwa mafunzo hayo ambayo yatakuwa na muendelezo katika htua yapili ambapo majaji watapewa fursa ya kusikiliza na kuamua mashauri katika wiki mbili zijazo.

Amekisifu Chuo cha Mahakama kwa kuwa msaada kwa kuandaa mafunzo hayo yanayoongozwa na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Jaji Salimu Masati.