Na Joyce Kasiki,Timesmajira online ,Dodoma
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo ameziagiza Halmashauri kuhakikisha maarifa yaliyopo kwenye sherehe ya wakulima na wafugaji (Nane Name) ,yanaongeza uwekezaji katika Kilimo,mifugo na uvuvi kwa ajili ya kukuza uchumi zaidi na kuwa na uchumi wa kati unaoendelea kuimarika ndani ya miaka mitano ijayo.
Akifungua sherehe hizo kwa Kanda ya Kati katika viwanja vya Nane Nane Nzuguni jijini Dodoma,Jafo amesema ,katika maonyesho hayo kuna maarifa mengi ambayo bado hayajaonyesha tija ya kutosha kwenye maeneo hayo muhimu kwa uchumi wa nchi.
“Bado tuna kazi kujenga uchumi wetu kwa kutegemea Kilimo mifugo na uvuvi ,maonyesho haya yakatumike vyema na kufika hadi kwa wananchi ili waongeze tija katika Kilimo ,mifugo na uvuvi.”amesema
Jafo
Amesema ,iwapo maarifa na Mafunzo yaliyopo katika maonyesho ya sherehe hizo angalau kwa asilimia 75 ni dhahiri nchi itapata mafanikio makubwa.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa