January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jack Grealish ‘Deal done’ Man City

MANCHESTER, England

KLABU ya Manchester City imemsajili kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa England, Jack Grealish kutoka Aston Villa kwa rekodi ya uhamisho huko Uingereza wa kitita cha fedha pauni milioni 1000.
Grealish, mwenye umri wa miaka 25, anajiunga na mabingwa wa Ligi Kuu England kwa kandarasi ya miaka sita na atavaa jezi namba 10 iliyoachwa hivi karibuni na legend Sergio Aguero aliyetimkia Barcelona.

Ada ya uhamisho wa Grealish inazidi pauni milioni 89 zilizolipwa na Manchester United kumsajili tena kiungo Paul Pogba kutoka Juventus mnamo 2016.

Akizungumza mara baada ya kumwaga wino, Grealish amesema Man City ni timu bora hivyo atajitahidi kadri ya uwezo wake kuhakikisha anaipa klabu hiyo kile kitu wanachokipenda.

“Man City ni timu bora na meneja anayechukuliwa kuwa bora ulimwenguni. Ni ndoto kutimia kuwa sehemu ya klabu,” amesema Grealish ambaye ni shabiki wa Manchester United kindakindaki.

Hat hivyo, mchezaji huyo anaweza kuichezea Man City katika mechi ya Jumamosi ya kesho Ngao ya Jamii dhidi ya Leicester City huko Wembley.