December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Issa Gavu atua Geita kuzindua kampeni leo

Na Mwandishi Wetu, Timesmajiraonline, Geita

KATIBU wa Halmashauri Kuu(NEC) Oganaisheni na Mjumbe wa Kamati Kuu, Issa Gavu amewasili mkoani Geita kwa ajili ya kuzindua rasmi Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Gavu amewasili mkoani Geita leo Novemba 20,2025 na baada ya kuwasili amefanya mazungumzo na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Geita kabla ya kuelekea katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi huo zitakazofanyika katika Viwanja vya Shilabela Geita Mjini.