January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Infantino minne tena Rais wa FIFA

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino amechaguliwa tena kuwa Rais wa Shirikisho hilo kwa muda wa miaka mingine minne kuanzia 2023 hadi 2027

Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo uliofanyika mjini Kigali, Rwanda Infantino amesema kuwa Rais wa FIFA ni heshima kubwa na furaha lakini ni jukumu kubwa pia.

“Kuwa Rais wa FIFA ni heshima kubwa, ni fursa ya ajabu. Pia ni jukumu kubwa. Hakika nimeguswa na sapoti yenu. Nawaahidi nitaendelea kuitumikia FIFA, kutumikia mpira wa miguu duniani kote, kutumikia vyama vyote 211 vya FIFA,” amesema Infantino.