Judith Ferdinand,Mwanza
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,imefanikiwa kukusanya zaidi ya bilioni 3.7,sawa na asilimia 25 ya lengo la makusudio ya makusanyo ya fedha za mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025.
Ambapo,Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela imekusudia kukusanya zaidi ya bilioni 14.9,katika bajeti ya mapato ya ndani kwa mwaka mzima wa fedha 2024/2025.Ambapo kuanzia Julai hadi Septemba 30,mwaka wa fedha 2024,imefanikiwa kukusanya kiasi hicho cha zaidi ya bilioni 3.7 sawa na asilimia 100 ya lengo la robo mwaka.
Hayo yamebainishwa Novemba 6,2024 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,Ummy Wayayu,akiwasilisha taarifa yake katika kikao ch Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo,kipindi ch robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025.
Wayayu alisema kuwa,katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo mwaka wa fedha 2024/2025,Halmashauri hiyo imeidhinishiwa kutumia zaidi ya bilioni 17.Ambapo kwa kipindi cha Julai-Septemba,2024,Halmashauri imepeleka zaidi ya bilioni 6.1 sawa na asilimia 36.1,kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
“Kwa mapato ya ndani robo ya kwanza,kiasi cha zaidi ya bilioni 2.4,zilielekezwa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata zetu,kati ya fedha hizo zaidi ya bilioni 1.0,ni fedha za mapato ya ndani zilizotolewa mwishoni mwa mwaka na fedha zilizovuka mwaka.Huku kiasi cha zaidi ya bilioni 1.3,ni fedha za mapato ya ndani kwa utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2024/2025,”alisema Wayayu.
Kati ya fedha hizo zaidi ya milioni 317.3, kwa ajili ya fidia ya ardhi,milioni 100 malipo ya Mkandarasi wa ujenzi wa barabara ya hospitali ya Wilaya ya Ilemela,milioni 40, kwa ajili ya uendelezaji wa jengo la mama na mtoto zahanati ya Nyakato,milioni 49 kwa ajili ya uzio shule ya msingi Kitangiri,milioni 35 kwa ajili ya umaliziaji wa bweni la watoto wenye mahitaji maalum shule ya msingi Buswelu.
Pia alisema kuwa,kwa robo ya kwanza zaidi ya bilioni 1.4,za mapato ya ndani zilielekezwa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo,ikiwa ni utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2024/2025, ikiwemo milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari Ilemela,zaidi ya milioni 262 kwa ajili ya mfuko wa wanawake,vijana na wenye ulemavu,milioni 140 ukamilishaji wa wodi ya wazazi zahanati ya Nyakato.
Hata hivyo kwa robo hiyo ya mwaka wa fedha 2024/2025, Halmashauri hiyo imepokea zaidi ya bilioni 3.7, kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kata,kati ya fedha hizo zaidi ya bilioni 2.0, ni fedha za miradi iliopokelewa mwishoni mwa mwaka 2023/2024 na kuelekeza kwenye miradi mbalimbali ikiwemo zaidi milioni 584 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari Masemele.
Huku zaidi ya bilioni 1.6 ni fedha za miradi ya ruzuku kutoka Serikali Kuu kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025,ambazo zimelekezwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa bajeti ya mwaka huo wa fedha ikiwemo zaidi ya bilioni 1.1, kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya lami Buswelu-Nyamadoke-Nyamh’ongolo Km 9.4 na Buswelu-Cocacola Km 3.3.
Msahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,Renatus Mulunga,ametoa rai kwa Madiwani na Watendaji wa Kata 19 na mitaa 171 ya halmashauri hiyo,kuhakikisha suala la ukusanyaji mapato liwe kipaumbele.
Pia Mulunga,alisema, Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela idadi ya wakazi inazidi kuongezeka kila mwaka,hivyo amewataka wataalamu wa mipango miji kuja na mpango wa kujenga madarasa ya ghorofa na kuoondokana na ujenzi wa madarasa ya kusambaa kama reli,ili ardhi iliopo iweze kutumika kwa miaka 50 ijayo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela,Wakili Mariam Msengi,amewahimiza Madiwani wa Halmashauri hiyo,kuendelea kusimamia suala la ukusanyaji mapato ya ndani,pamoja na fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na inakamilika kwa wakati.
Kwa upande wao baadhi ya Madiwani wa Halmasahauri hiyo akiwemo Diwani wa Kata ya Kiseke,Mwevi Mwevi,ambaye amepongeza taarifa hayo huku akisisitiza Mkurugenzi kuhakikisha eneo la zahanati ya Lubala,iliopo Kata ya Kitangiri kiwanja hicho kinapata hati miliki yenye jina la Halmashauri.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba