Na Judith Ferdinand, Timesmajira Online,Mwanza
Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza inatarajia kupokea Mwenge Julai 14,2023 ukitokea katika Wilaya ya Ukerewe ambapo ukiwa wilayani hapo unatarajiwa kukimbizwa umbali wa kilomita 57.
Hayo yamebainishwa katika taarifa iliyotolewa na Halmshauri ya Manispaa ya Ilemela ambayo imeeleza kuwa siku hiyo Mwenge wa Uhuru utapokelewa bandari ya Nyehunge ukitokea wilayani Ukerewe na utakesha katika uwanja wa Furahisha wilayani humo jijini Mwanza.
Mwenge wa Uhuru wilayani hapo utapita katika miradi 6 yenye thamani ya bilioni 1.35 na utakagua shughuli tano pia utazindua miradi miwili yenye thamani ya bilioni 1.19.
Pia kwa mwaka huu katika wilaya hiyo Mwenge wa Uhuru utaweka jiwe la msingi katika mradi mmoja wenye thamani ya milioni 100.
Aidha mbali na hayo pia Mwenge wa Uhuru utakagua miradi mitatu yenye thamani ya milioni 50.9, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu yam bio za Mwenge huo ni “Tunza mazingira ,okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai,kwa uchumi wa taifa”.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi