Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
WILAYA YA ILALA inatarajia kupanda miti milioni 1.5 kwa ajili ya kampeni ya utunzaji Mazingira na kuhifadhi vyanzo vya maji .
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija katika uzinduzi wa siku ya MAZINGIRA Duniani ambapo Wilaya ya Ilala imezindua kwa kufanya usafi na kupanda miti ndani ya Wilaya llala.
Uzinduzi huo wa wiki ya Mazingira Wilaya ya Ilala ulizinduliwa Dar es Salaam Juni 02/2022 katika Kata ya Gerezani Kariakoo ambapo wadau wa Mazingira na Wakandarasi wa Kampuni za uzoaji taka walipongezwa sambamba na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kazi nzuri ya kulipendezesha Jiji hilo katika Mazingira ya usafi na kuifanya Wilaya ya Ilala kupendeza.
“Kampeni yetu ya utunzaji Mazingira katika Wilaya ya Ilala tunatarajia kupanda miti milioni 1.5 naomba Wananchi wote tupande miti katika maeneo yetu hii ni kampeni endelevu kwa kila Kata kila kaya na kila mmoja wetu aone fahari kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi” alisema Ng’wilabuzu.
Mkuu wa Wilaya Ng’wilabuzu amewataka Wananchi wa Wilaya ya Ilala pia kupanda miti ya vivuli pamoja na miti ya matunda katika maeneo yao.
Wakati huo huo Ludigija aliwapongeza Wakandarasi wa Kampuni za usafi ambao wanalipendezesha Jiji hilo kwa usafi na baadhi ya kampuni za usafi zilipewa pongezi kwa kutambua mchango wao kampuni hizo ni KAJENJELE,KIMWEDE na SATEKI za jijini Dar Salaam.
Alisema Jiji la Dar es Salaam limeshika nafasi ya sita kwa usafi Barani Afrika, ni Jiji Bora sura ya nchi yetu TANZANIA inabebwa na Jiji hilo hususani Wilaya ya Ilala .
Katika hatua nyingine Ludigija amewataka Waendesha Bodaboda na Bajaj wa Wilaya ya Ilala kufuata taratibu katika vituo vyao vya kazi walivyopangiwa hili Halmashauri ya Jiji Dar es Salaam iweze kupendeza .
Pia aliwataka Waendesha Bodaboda na Bajaj kufuata kanuni za usafi katika vituo vyao walivyopangiwa kwa kufanya usafi kila wakati na vyombo vya usafiri ikiwemo Daladala kufunga vifaa Maalum vya kuifadhia taka taka.
Kwa upande wake Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto alisema Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inajivunia kwa usafi kwa Sasa miaka sita Ilala amna ugonjwa wa kipindupindu ni juhudi kubwa zilizofanywa na Watendaji wa Wilaya hiyo pamoja na MAAFISA Afya katika kitunza Mazingira.
Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam RAJABU NGODA alisema katika wiki ya Madhimisho ya Mazingira Duniani kuanzia Juni Mosi mpaka Juni tano Halmashauri ya Jiji hilo imejipanga kutoa elimu ya usafi wa Mazingira katika shule Kumi pamoja na Kampeni endelevu ya Upandaji miti ya matunda na kivuli.
More Stories
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti