Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo,amesema mikakati ya wilaya ya Ilala kujenga masoko ya kisasa shule ,na vituo vya afya kutokana na halmashauri hiyo kukusanya Mapato mengi kuvuka lengo .
Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo ,amesema hayo katika Kongamano la mwaka mmoja la Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Ilala Said Sidde toka achaguliwe kushika madaraka wilaya hiyo.
“Malengo ya wilaya Ilala mikakati tuliojiwekea kwa sasa shule zote za gorofa na vituo vya afya vinakamilika kwa wakati pesa zipo ,bajeti yetu Ilala shilingi Bilioni 87 lakini tumeweza kuvuka lengo baada kubana mianya ya ulaji pesa za Serikali Mapato yameongezeka katika kipindi cha miezi mitatu tumeweza kukusanya Mapato ya Halmashauri shilingi bilioni 2.5 “alisema Mpogolo.
Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo, alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Jomaary Mrisho Satura ,Madiwani na watendaji kwa kazi nzuri ya kukusanya Mapato vizuri ya Serikali amewataka wakaze buti waendelee na mikakati hiyo ya ukusanyaji fedha vizuri halmashauri hiyo iweze kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo katika utekelezaji wa Ilani ya chama.
Alisema mikakati waliojiwekea kwa sasa kujenga soko la kisasa Ilala,Gongolamboto na Chanika ili yaweze kutoa huduma kwa wananchi wa eneo hilo ambapo aliwataka wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapunduzi.
Aidha alisema Serikali imeshatoa zaidi ya billion 200 kwa ajili ya miradi ya maendeleo amewataka waisimamie na kutekeleza katika maeneo yao na kuitangaza kwa wananchi .
Alisema jukumu la Halmashauri kusimamia haki za wafanyabishara,Bodaboda,Mama lishe sio kuchukua bidhaa zao Serikali ya wilaya Ilala itasimamia haki na kama watakuwa hawatendewi haki watoe taarifa.
Wakati huo huo aliwapongeza Wabunge,madiwani kupitisha kanda kwa ajili ya kusogeza huduma bora kwa wananchi ambapo Ofisi za kanda zote zinatoa huduma za Serikali ikiwemo kutatua migogoro ya ardhi na mingineyo ambapo katika Ofisi hizo za Kanda kuna maafisa wote wa Serikali watakuhudumia vizuri.
Akizungumzia mwaka mmoja wa Mwenyekiti wa CCM WILAYA YA ILALA SAID SIDDE alisema Said Sidde anaushirikiano mkubwa chama na Serikali pamoja na Kamati yake ya siasa nzuri na Wabunge wa Wilaya ya Ilala wote wazuri wameaminiwa na Serikali na sasa wamepewa madaraka makubwa ya uongozi.
Mwenyekiti wa CCM kata ya Kisutu MURTAZA DARUGAR, alimpongeza Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Ilala Said Sidde kwa uongozi wake bora wa chama hicho na kusimamia haki na kutatua migogoro mbalimbali katika ziara zake.
Mwenyekiti MURTAZA DARUGAR alisema wanaunga mkono juhudu za Rais katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi anafanya kazi kubwa kuwatumikia wananchi.
Mbunge wa Jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli, alisema mikakati ya chama cha Mapinduzi CCM kuakikisha ccm inashika dola katika chaguzi zote.
Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu alisema Mwenyekiti Said Sidde ni Mwenyekiti Bingwa anaunga mkono juhudi za Serikali katika kipindi cha mwaka mmoja ameweza kuitisha mkutano wa hadhara kuzungumzia Suala la Bandari pia katika kipindi cha mwaka mmoja ameweza kuitisha Dua maalum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan aweze kutekeleza majukumu yake vizuri na kutekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilala Said Sidde alisema katika kipindi chake cha uongozi Ilala inasonga mbele Mapato yameongezeka,vituo vya afya vinajengwa anashirikiana na Serikali kuakikisha malengo waliojiwekea yanafikia ikiwemo kusimama miradi mbali mbali ya maendeleo sekta ya afya ,elimu pamoja na miundombinu ya Barabara.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Ilala Juma Mizungu alisema katika jumuiya wanashirikiana na chama katika utekelezaji wa majukumu yao pamoja na Jumuiya ya Wazazi na UWT ambapo alisema Umoja wa vijana wanajukumu kubwa la kumsaidia Rais katika kusimamia miradi ya Serikali.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu