Na Penina Malundo, timesmajira
CHUO cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimetoa msaada wa mahitaji muhimu kwa waathirika wa maporomoko ya tope kutoka milima ya Hanang yaliyotokea Disemba 3,2023 kwenye mji mdogo wa Katesh.
Akizungumza baada ya kuwasilisha msaada huo,Afisa Habari wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha mwishoni mwa wiki,Dkt. Michael Sam,amesema wafanyakazi wa chuo cha IFM waliguswa kwa kipekee baada ya kutokea maporomoko hayo kwa wananchi wa hanang hivyo kuamua kwenda kuwafariji.
Amesema wameweza kukabidhi vitu mbalimbali ikiwemo sukari,unga wa dona,Maharage,Kandambili,Pencel,Peni,Mfuko yenye nguo,Mfuko wa Viatu,Mahindi pamoja na Miche ya Sabuni.
Dkt.Sam amesema vitu hivyo vimetolewa na wafanyakazi wa IFM kwa kujichangisha kidogo kidogo kwa lengo la kutimiza adhima yao ya kusaidia waathirika hao.
”Tuliguswa kwa kipekee baada ya kutokea mafuriko ya hanang, Wafanyakazi wa IFM waliguswa na kuona kuja haja ya kuwapatia msaada kama jamii ya Watanzania,”amesema na kuongeza
”Tulianza zamani mchakato huu wa kuchangia kwa lengo la kununua vitu na kuja kuwakabidhi watanzania wenzetu na kuja kuwafariji,”amesema.
Ametoa wito kwa watanzania kuendelea kuwagusa wananchi walioathirika na maporomoko hayo kwa kuwapatia misaada mbalimbali kwani bado baadhi yao wanaishi kwa ndugu na jamaa.
”Tunahamasisha wengine wachangie kama tulivyohamasisha sisi wafanyakazi wa IFM tuendelee kutoa sapoti kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika shughuli hii kwani wote ni watanzania wenzetu,”amesema.
Kwa Upande wake,Mwakilishi wa Wafanyakazi wa IFM kwenye kukusanya michango kwa wahanga wa Hanang,Juma Kibacha alisema kwa taasisi kufanya hivi wanarudisha shukrani kwa jamii.”Natoa wito kwa taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizoza kiserikali tuone hili kama ni letu na kuwasaidia waathirika hao,”amesema.
Aidha amesema takribani Milioni 5 zimechangwa na wafanyakazi hao huku wakiamini kuwa msaada huo waliotoa utawasaidia waathirika hao pale walipokwam
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi