Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
RASMI klabu ya Simba imemtambulisha beki wao mpya wa kati Ibrahim Ame aliyesaini kandarasi ya miaka mitatu kuitumikia klabu hiyo akitokea Coastal Union.
Tetesi za Simba kumalizana na beki hiyo zilianza kuwekwa wazi toka mwanzoni mwa mwezi huu baada ya kile kilichotajwa kuwa kuwazunguka wapinzani wao Yanga ambao nao walikuwa wakiwania saini ya beki huyo.
Licha ya kuwa kwa muda mrefu mchezaji huyo ambaye alikuwa akicheza pacha na beki mpya wa Yanga, Bakari Mwamyeto kuwa kwenye mipango ya Yanga lakini imeelezwa Simba kumdaka wakati alimkuwa ameshamalizana nao kila kitu ili kuendeleza pacha ya mabeki hao wawili na kuimalisha safu yao ya ulinzi.
Toka mwezi Mei ilielezwa vigogo ya Yanga walianza kuzungumza na wakala wa beki huyo ambaye pia ni wakala wa Mwanyeto baada ya kuwa na wasiwasi kuwa huenda Simba ingevuruga mipango yao kwa Mwamnyeto.
Ilielezwa kuwa, baada ya Simba kupata taarifa kuwa Ame anakuja Dar akitokea Zanzibar ambako alikwenda kwa ajili ya mapumziko, walimfuata bandarini na kumpokea kisha kwenda kufanya nae makubaliano licha ya uwa wakala wa mchezaji huyo alikuwa kijua kuwa anakwenda kusaini Yanga baada ya kumalizana nao.
Beki huyo sasa ana kazi kubwa ya kuhakikisha anagombania namba na wakongwe Erasto Nyoni, Pascal Wawa pamoja na Kennedy Juma ambaye ameonesha kiwango bora.
Ame anakuwa mchezaji wa sita kutambulishwa baada ya klabu hiyo kumtambulisha winga Benard Morrison, Charles Ilanfya, beki Joash Onyango, David Kameta na kiungo Larry Bwalya.
More Stories
Rais Samia atia mkono mchezo wa masumbwi Tanzania
Chino bingwa mpya wa IBA Intercontinental Championship
Mnzava apania kuwapeleka vijana Simba na Yanga